Friday 30 December 2016

Rc Ndikilo ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo kuondoka haraka

kau
 
Kutokana na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini ,mbunge wa chalinze Mh RIDHIWANI KIKWETE ameiomba serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro iyo.
Mkutano huu unafuatia hali mbaya ya mapigani baina ya wakulima na watugaji kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari. Mapigano hayo ambayo yalianza siku nyingi , sasa yamefika pabaya baada ya matukio ya watu kuuawa, kuvunjwa viungo na hata wengine kukimbia makwao kwa sababu ya kile kilichoitwa kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafigaji.
kama ilivyoandikwa kwenye vitabu va dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha mbunge ridhiwani kikapokewa vyema na mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30 ,kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo,”Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi,haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa”…alisema Ndikilo
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza kabla ya mkuu wa mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo hajakaribishwa kuzungunza na Wananchi , Mbunge wa Chalinze Bwana Ridhiwani Kikwete alisema katika kijiji hicho kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi kinyume cha Taratibu hivyo kutumia njia ya kijiji kama njia halali ya kupeleka mifugo yao mto Ruvu kuwanywesha maji. Vitendo hivyo vimepelekea wananchi wengi kupoteza mazao yao ; jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga,hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo..
Rc Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo. Mifugo imekuwa mingi sana katika eneo hili la kitonga na mkoa wa pwani , mkuu wa mkoa alisema. Kwa mujibu wa sensa iliyofanywa kwa kuwahoji wafugaji wenyewe,walidai kuwa wana ngombe wapatao laki 5,lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho. ” hata kama ukweli ndiyo uo , eneo la kufuga mkoa wa Pwani linauwezo wa kuchukua Ng’ombe laki 2 na Nusu. Hivyo kuna ziada ya mifugo laki 2 na nusu.
Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo. “Operesheni ya kuondoa mifugo katika Bonde la Ihefi ndiyo iliyofungua mlango huo. Wafugajo walitengewa maeneo Lindi lakini wengi walishuka pwani kwa kuona Maji na majani.”, alisema Mkuu wa Mkoa. Sasa muda umefika tusimamie taratibu tulizojiwekea.
Akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima ndikilo amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa amani na upendo. Katika Mkutano huo pia Mkuu wa Mkoa wa Pwani alitumia nafasi kuwaonya wote wanaojiona kuwa wako juu ya sheria na pia wale wanaojidai kuwa wao ndiyo mababa wa Kitonga kwa kuwa mbele ya sheria hakuna aliyejuu. Alitoa tahadhari kuwa atashughulika na hap wote na onyo kali kwa kiongozi wao Bwana Leki ambaye inasemekana yeye ndiyo anayewaita wenzake na kuwapa kibuli.
kwa upande wake mbunge wa chalinze mara baada ya kauli ya mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoingia kinyemela.
wanakijiji cha Kitoga wakisikiliza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza kwa wananchi katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa maelekezo kwa wanakijiji baada ya kufika katika kijiji cha Kitonga kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na watendaji mkoa wa Pwani baada ya mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza

No comments:

Post a Comment