Friday 23 December 2016

Upinzani na serikali waafikiana DRC

Bwana Kabila amekataa kuachia madaraka hatua iliyosababisha maandamano mabaya
Viongozi wa Upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanasema kuwa muafaka umeafikiwa na chama tawala kuhusiana ubadilishanaji mamlaka.
Katika makubaliano yaliyoongozwa na Kanisa Katoliki, Rais Joseph Kabila atasalia mamlakani hadi mwisho wa mwaka ujao wa 2017, licha ya muhula wake kumalizika rasmi.

Waziri mkuu mpya atachaguliwa kutoka mrengo wa upinzani, na muafaka huo utaalindwa na kinara mkuu wa upinzani, Etienne Tshi-sekedi.

Bwana Kabila amehudumu kwa mihula miwili sawa na katiba ya taifa hilo, lakini uchaguzi mkuu umecheleweshwa.
Bwana Kabila amekataa kuachia madaraka hatua iliyosababisha maandamano mabaya katika barabara za miji ya taifa hilo.
Serikali imekubaliana na mapatano hayo ambayo upinzani inasema kuwa yatatiwa saini hatimaye leo Ijumaa.

No comments:

Post a Comment