Tuesday 27 December 2016

Kaike Siraju: Francis Cheka anastahili kufanyiwa uchunguzi wa akili yake

 Bondia Francis Cheka

Promota wa ngumi nchini Kaike Siraju, ameibuka na kumtaja bondia Francis Cheka kama mtu anayestahili kufanyiwa uchunguzi wa akili yake kutokana na kutopanda ulingoni Jumapili hii katika pambano lake na bondia Abdallah Pazi (Dullah Mbabe.

Kaike ambaye ndiye aliyekuwa Promota wa pambano hilo, ameelezea kusikitishwa kwake na kitendo kilichofanywa na Cheka, huku akisisitiza kuwa Cheka anatakiwa kupimwa akili kwa madai kuwa kitendo alichokifanya hakiwezi kufanywa na binadamu mwenye akili timamu.
Akizungumzia madai ya Cheka kwamba alikuwa hajalipwa, Siraju amesema tayari alikuwa amekwishatoa pesa ya utangulizi shilingi milioni 4 na kwa mujibu wa taratibu za mapambano, alipaswa kumaliziwa pesa yake muda ambao anapanda ulingoni, lakini Cheka aligoma tangu mapema kucheza pambano hilo licha ya kuwa walikuwa wamekwisha kubaliana kila kitu.

 Kaike Siraju

"Mimi nimesaini kila kitu, mikataba yote ipo, Cheka kachukua milioni nne, utaratibu ni kwamba pesa nyingine anapaswa kuchukua siku ya pambano kabla ya kupanda ulingoni, kwahili sitakubali kudhalilika, lazima nitachukua hatua za kumdisplini.... ..Cheka afanyiwe CT Scan, lazima atakuwa na matatizo, haiwezekani mtu mwenye akili timamu ufanye jambo kama hilo.

 Najua kuna watu wako nyuma ya pazia, wanamshawishi asicheze mapambano yangu ili wao ndiyo waje kuingiza pesa, kuna watu nawajua sasa hao watu waje wamtetee na mahakamani" Amesema Kaike
Kuhusiana na madai kuwa Cheka alikuwa akimdai pesa, Kaike amemtaka Cheka kujitokeza hadharani na kusema ukweli kama kuna hela nyingine anayomdai na aseme ni kiasi gani

 Francis Cheka
Napenda mfahamu nilikosa imani kabisa na huyu promota siraju kaike kwa sababu niliwahi kucheza mechi na mthailand Kiatchai Singwancha aliiandaa yeye hela yangu sijalipwa mpaka leo hata mzee wang Emmanuel Mlundwa analifahamu na bado namdai.Ndio maana safari hii nilitaka anipe hata nusu lakini hakufanya hivyo kwakua nilihofia isije ikajitokeza kama mechi hii nilishuka ulingoni hela yang sikulipwa nauli ya kurudi Morogoro nilisaidiwa na wasamalia wemaa.

Cheka pia aliweka wazi utaratibu wake wa kucheza mapambano kwa sasa na kusema "Nimeweka utaratibu sipandi ulingoni bila kumaliziwa pesa yangu mm nimeshakua maarufu tayar nipo kikazi zaidi".

No comments:

Post a Comment