Thursday 29 December 2016

Nyumba ya Carlos Tevez yaibiwa akiwa katika ndoa

Carlos Tevez na mkewe Vanesa Mansila katika harusi yao huko Uruguay
Wezi walivunja na kuingia katika nyumba ya aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez viungani mwa mji wa Bueno Aires nchini Argentina siku ya Jumapili na kuiba wakati nyota huyo alipokuwa nchini Uruguay kufunga ndoa.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa Tevez hakuwasilisha ripoti kwa polisi kuhusu wizi huo hivyobasi haijulikani ni nini kilichoibiwa.
Tevez na mke wake tayari wameondoka na kuelekea Mexico kwa fungate yao.

Polisi wanasema kwamba waligundua kuhusu wizi huo siku ya Jumanne baada ya kuwaona wanahabari wamekusanyika nje ya nyumba hiyo ya nyota huyo wa Argentina.
Wanasema kuwa wezi wengi waliingia katika nyumba hiyo ambayo Tevez na familia yake walikuwa wamekodi huku wakisubiri nyumba yao ambayo ilikuwa inafanyiwa ukarabati.

Inadaiwa wezi hao waliingia nyumba hiyo kupitia eneo ambalo ukarabati huo ulikuwa ukifanywa.
Baada ya Tevez kuarifiwa kuhusu wizi huo, alirudi nyumbani kwake kwa helikopta .
Aliukuta mlango wa nyumba yake uko wazi huku vitu vikiwa vimepekuliwa.

Tevez baadaye alisafiri kuelekea Mexico kama alivyopanga kwa fungate yake na mpenziwe wa utotoni Vanesa Masilla.
Wawili hao waliokutana wakiwa na umri wa miaka 13 na ambao wana wasichana wawili, walifunga ndoa katika sherehe ya kawaida siku ya Ahamisi mjini Bueno Aires.

No comments:

Post a Comment