Saturday 31 December 2016

Solo Thang ajitetea kuhusu Chid Benz

SoloThang
Msanii mkongwe wa Hip Hop Bongo Solo Thang amejitetea kuhusu uamuzi wake wa kurekodi video akiwa na Chid Benz na kusema alichokifanya si 'kumchoresha' bali ni kumfariji na kutomnyanyapaa maana Chid mwenyewe ndiye aliyeomba kitu hicho kifanyike
Baadhi ya wadau wa muziki wa Bongo Fleva walitoa kauli zilizoonesha kulaumu kurekodiwa kwa Chid Benz akiwa katika hali ya kudhoofika wakidai kuwa ni kumdhalilisha.
Kamera ya eNewz ilmtafuta Solo Thang na kumuuliza nia yake ya kupost video hiyo ilikuwa ni nini? Solo alisema kuwa hakukusudia kumchoresha Chid Benz bali Chidi mwenyewe ndiye aliyetaka kurekodiwa video baada ya kukutana naye.

“Chid ni mdogo wa rafiki yangu na nilimfahamu zamani sana kabla hata hajaanza kuimba. Hivyo tuna historia ndefu kidogo, Chid kwa sasa huwa hapigi picha na watu, lakini tulipoonana ni yeye mwenyewe ndiye alitaka tushoot ile video, Lakini sikuwa na nia ya kumchoresha” Alisema Solo Thang.

Pia Solo Thang amewaambia watanzania kuwa waache kumlaumu Chid Benz na baadala yake wamsaidie, na wasichoke kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment