Saturday 24 December 2016

UN yashindwa kuiwekea Sudan Kusini vikwazo

Mapigano yameshuhudiwa nchini Sudan Kusini tangu Disemba mwaka 2013
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekataa azimio lililoungwa mkono na Marekani la kuiwekea vikwazo vya silaha taifa la Sudan Kusini, licha na onnyo kuwa huenda taifa hilo likakumbwa na mauaji ya halaiki.
Azimio hilo lilipata kura saba ya kura 15 na kukosa kufikisha kura tisa ambazo zinahitajika kupitishwa azimio.
Nchi nane zikiwemo Urusi,China na Japan hazikupiga kura.

Mapigano kati ya vikosi watiifu kwa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na makamu wa rais aliyefutwa kazi Riek Machar, yalizuka mwezi Disemba mwaka 2013 na kusababisha nchi hiyo kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

No comments:

Post a Comment