Friday 23 December 2016

Cheka asema hawezi kuuza pambano


Bondia Francis Cheka ambaye Jumamosi iliyopita alipigwa kwa TKO nchini India, amesema chanzo cha kutangazwa kupigwa ni uamuzi wenye utata.
Cheka alipigwa na Vijender Singh raundi ya tatu ya pambano la raundi 12 la uzani wa Super middle 76 kuwania ubingwa wa Mabara wa WBO lililofanyika mjini New Delhi usiku wa Desemba 18.
Katika pambano hilo, Cheka alionekana bado yuko fiti akiwa kwenye kona yake wakati mpinzani wake akimlalamikia mwamuzi ambaye sekunde chache baadaye alionyesha ishara ya kumaliza pambano na kumpa Singh ushindi.
“Nilipaliwa na mate nikaanza kukohoa mfululizo, nilitema mouth gurd ‘kilinda ulimi’ na kusogea kwenye kona yangu nimuombe kocha (Abdallah Salehe) anipe mouth gurd nyingine.

“Nikiwa katika harakati za kuomba mouth gurd, nikashangaa kuona refarii anamnyanyua Singh na kumtangaza kuwa bingwa na mimi nimepigwa kwa TKO, kiukweli sikuelewa lakini refarii ndiye mwenye matokeo ya mwisho,” anasema Cheka. Anasema alitaka kubadilisha kilinda ulimi kwa kuwa kile alichovaa awali kilikuwa kidogo hivyo kikawa kinasababisha ajaze mate mdomoni.

No comments:

Post a Comment