Thursday 29 December 2016

Tambwe kuwakimbiza Msuva, na Kichuya.

  Image result for Hamis tambwe
Mshambuliaji wa Yanga raia wa Burundi Amis Tambwe, ameingilia rasmi vita ya ufungaji bora msimu huu wa ligi kati ya Saimon Msuva ambaye yuko naye Yanga na Shiza Kichuya ambaye anakipiga kwa watani zao wa jadi, Simba SC.
Hatua hiyo ni baada ya Jana Mrundi huyo kupiga bao lake la 9 katika ligi kuu Msimu huu katika ushindi wa mabao 4-0 ambao Yanga iliupata dhidi ya Ndanda FC.
Bao hilo limemfanya kuwa sawa na vijana hao wawili Kichuya na Msuva ambao ndiyo waliokuwa kwenye mbio za ufungaji bora.

Shiza ana nafasi ya kuwakimbia wana Jangwani hao endapo leo atafunga katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting kabla timu hizo hazijatimkia kwenye michuano ya Mapinduzi visiwani Zanzibar.
Hadi mzunguko wa Kwanza unamalizika, Kichuya  ndiye aliyekuwa kileleni akifuatiwa na Tambwe na Msuva ambao wote walikuwa na mabao 7 kila mmoja lakini baada ya mzunguko wa pili kuanza, Kichuya hajafunga bao lolote, huku Tambwe akifunga bao moja moja katika michezo miwili, na Msuva akifunga mawili katika mchezo mmoja.
Ikumbukwe kuwa Tambwe ndiye aliyekuwa mfungaji bora msimu uliopita, akifunga jumla ya mabao 21. Je ataweza kutetea taji lake hilo la ufungaji bora.
Ni vita kati yake, Msuva, na Kichuya.

No comments:

Post a Comment