Wednesday 28 December 2016

Nyota wa Filamu ya Star Wars,Carrie Fisher amefariki dunia

Nyota wa Filamu ya Star Wars,Carrie Fisher aaga dunia
Fisher , al maaruf kama Princess Leyla katika sinema hiyo ya Star Wars alikumbwa na mshtuko wa moyo akiwa safarini kwa ndege na kupelekwa hospitalini juma lililopita .

Baadaye aliripotiwa kuwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji kwa niaba ya familia ya Fisher ni kuwa nyota huyo alipoteza maisha mapema asubuhi ya siku ya Jumatano.

Waigizaji wenzake na watu maarufu katika ulimwengu wa sanaa walituma ujumbe wa rambi rambi .

Fisher atakumbukwa katika mchango wake katika ulimwengu wa sanaa hasa katika filamu za 'Blue Brothers','Hannah anda Her Sisters' na ''When Harry met Sally

No comments:

Post a Comment