Monday 26 December 2016

 Pepe kutoka Euro 4milion hadi 10milion na dili la China

Pepe anategemewa kusepa kwenye club ya Real Madrid na hategemewi kupunguza mshahara wake zaidi ya kuongeza mara mbili yake na zaidi.

Super agent Jorge Mendes amefanya mazungumzo yasiyo rasmi kwa uwezekano wa mchezaji wake huyo kujiunga na club ilioyopo kwenye Chinese Super League kwa mshahara mkubwa mara mbili zaidi anaoupata sasa hivi Real Madrid.
Hii itakua kitu kinigne kikubwa kwa Chinese Super League kwa kumpata mchezaji maarufu ambaye ametoka kushinda kombe la club bingwa dunia na ulaya. Taarifa zinasema kwamba Pepe yupo tayari 50% kujiunga na club ya Hebei Fortune.

Sasa hivi offer iliypripotiwa kwa ajili ya Pepe ni kiasi cha Euro milioni 10 baada ya kodi wakati akiwa Real Madrid anapata Euro milioni 4.5 baada ya kodi.

No comments:

Post a Comment