Monday 26 December 2016

Mwambusi akiri kuzidiwa mbinu na African Lyon

Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga Juma Mwambusi amekiri kizidiwa mbinu katika mchezo dhidi ya African Lyon uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mwambusi amesema, wachezaji wa African Lyon wamecheza kwa kiwango kizuri katika mchezo huo hali iliyopelekea wachezaji wake kuzidiwa mbinu na kukubali sare ya bao 1-1 katika mchezo huo.

Kwa upande wake Kocha wa African Lyon Charles Otieno amesema, siri kubwa ya wachezaji wake kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo ni kufanya mashambulizi ya ghafla hali iliyowapelekea wapinzani wao kushindwa kupata ushindi katika mchezo huo.
Lyon walitangulia kupata bao kupitia kwa Ludovick lakini Tambwe alisawazisha bao hilo na kuiokoa timu yake isipoteze mchezo.
Timu ya Yanga ambayo ndio mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea kusalia katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 37 nyuma ya vinara wa Ligi hiyo Simba yenye Pointi 41.


No comments:

Post a Comment