Wednesday 28 December 2016

Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita anatarajia kuwa mgeni rasmi katika fainali za kuwania Kombe la Diwani wa Tabata

meya-wa-dar-isaya-mwita
Na Mwandishi Wetu
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita anatarajia kuwa mgeni rasmi katika fainali za kuwania Kombe la Diwani wa Tabata yanayotarajia kuanza Januari nane mwakani kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Tabata.
Akizungumza juzi, Diwani wa Kata ya Tabata, Patrick Assenga alisema ufunguzi wa mashindano hayo mgeni rasmi anatarajia kuwa Meya wa Ilala Charles Kuyeko.
Assenga alisema kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, Januari 3 anatarajia kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki 16 vikiwemo jezi na mipira  kwa washiriki.
Aseenga alisema mashindano hayo yatashirikisha timu mbili za mitaa nane ambako mitaa yenyewe ni pamoja na Tabata, Kisiwani, Msimbazi, Msimbazi Magharibi, Mtambani, Mandela, Matumbi na Tenge.
Assenga ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Mipango miji wa jiji la Dar es Salaam alitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza ni ng’ombe mkubwa na mpira, mshindi wa pili atazawadiwa ng’ombe na mpira na mshindi wa tatu atazawadiwa mipira na jezi.
Aidha Assenga alisema katika ufunguzi wa mashindano hayo atawashirikisha wachezaji wa zamani kama akina Jella Mtagwa, Peter Tino na wengineo kwa lengo la kuwapa heshima kwa waliyoifanyia Tanzania miaka iliyopita.
Assenga alisema hamasa hiyo itasaidia wachezaji wa sasa kuongeza hamasa kwa akina Mbwana Samatta ili wasijutie mchezo huo

No comments:

Post a Comment