Tuesday 27 December 2016

Kilichofuata baada ya Kocha wa Samatta kutimuliwa KRC Genk

Uongozi wa KRC Genk umesema umelazimika kumtupia virago kocha wake Peter Maes kwa kuwa matokeo yalikuwa yakizidi kuporomoka.
 
Genk ndiyo klabu anayoichezea Mtanzania Mbwana Samatta na ndiye aliyependekeza kusajiliwa kwa nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Umesema baada ya Maes kuondoka, msaidizi wake Rudi Cossey ndiye atachukua nafasi ya kocha huyo hadi itakapotangazwa halo baadaye.
Mara ya mwisho, Genk ilipata ushindi kwenye Ligi Kuu ya Ubelgiji Novemba 19, jambo ambalo limeufanya uongozi ho kukata tamaa.

No comments:

Post a Comment