Tuesday 27 December 2016

Wabunge 29, wakikacha chama tawala Korea Kusini

Rais wa Korea kusini Park Geun-hye
Wabunge 29 wa Bunge la Korea kusini wamejiondoa katika chama tawala nchini humo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia tuhuma za rushwa ambazo pia zinamgusa Rais wa nchi hiyo Park Geun-hye kwa mashtaka ya kutumia madaraka vibaya.
Hatua hiyo imekuja ikiwa imebaki miezi michache kufanyika kwa uchaguzi wa Rais.
Wabunge hao wanatarajiwa kuunda chama kingine kipya na upo uwezekano wa kumtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake Ban Ki-Moon, kuwa mgombea wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment