Mkurugenzi
Mtendaji wa Eco Bank, Enock Osei Safi (kushoto) akimkabidhi msaada wa
vifaa vya uzazi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dk Khamis Kigwangalla (wa pili kushoto), Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk Amani Malimana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk Amani Malima (aliyesimama) akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa ECO Bank, Enock Osei Safi (aliyesimama) akihutubia kwenye hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Khamis Kigwangalla akihutubia kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wajawazito walioshiriki hafla ya kukabidhi vifaa vya kujifungua vilivyotolewa na benki ya Eco Bank.
Na Mwandishi Wetu
UPUNGUFU
wa vituo vya afya na watoa huduma wasiokuwa na ujuzi na stadi za kuokoa
maisha ni miongoni mwa vyanzo vinavyochangia kasi ndogo ya kuondokana
na vifo vya uzazi na watoto wa umri wa chini ya mwezi mmoja.
Hayo
yalisemwa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Khamis Kigwangalla, alipokuwa
akipokea msaada wa vifaa tiba vya uzazi kutoka Eco bank.
Vifaa
hivyo vilivyotolewa kwa hospitali ya rufaa ya Temeke jijini Dar es
Salaam wakati benki hiyo ikiadhimisha siku yao ambayo mwaka huu kauli
mbiu ilisema, ‘kuboresha huduma kwa wajawazito barani Afrika.’
“Katika
kulipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo la vifo vinavyotokana na uzazi,
jawabu lipo katika kuongeza vituo vya afya na watoa huduma wenye ujuzi
na stadi za kuokoa maisha pamoja na vifaa tiba vya kutosha,” alisema.
Hata
hivyo, Dk Kigwangalah alisema hali si nzuri kwa upande wa vifo vya
uzazi na watoto wenye umri wa mwezi mmoja kutokana na takwimu zilizopo
kuonyesha kuwapo kwa kasi ndogo katika udhibiti wake katika kipindi cha
miaka 20 iliyopita.
Alisema
takwimu za vifo hivyo zinaonesha kuwa mwaka 1996 kulikuwa na vifo 529
vilivyopungua kufikia 432 kwa vizazi hai 100,000 katika kipindi cha
mwaka 2012, ikiwa ni sawa na vifo 7,500 kwa mwaka mmoja.
Kwa
upande mwingine, Dk Kigwangalla alisema vifo vya watoto wachanga wenye
umri wa chini ya mwezi mmoja ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili
afya ya uzazi kutokana na takwimu kuonesha kuwapo (vifo) 21 kwa kila
vizazi hai 1,000
Akizungumza
katika halfa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Eco Bank, Enoch Osei Safi
alisema siku ya benki hiyo inaadhimishwa katika nchi 33 za Afrika na
kushirikisha utoaji misaada kulingana na mahitaji na mazingira ya nchi
husika.
“Tumeazimia
kuadhimisha siku yetu kwa kuipatia hospitali hii vifaa tiba vya uzazi
ikiwa ni baada ya mashauriano ya pamoja yaliyotuwezesha kuwapo upungufu
katika eneo hilo,” alisema.
Kwa
mujibu wa Safi, Eco Bank iliichagua hospitali ya rufaa ya Temeke
kutokana na namna inavyowahudumia watu wengi kutoka maeneo tofauti ya
jijini Dar es Salaam ikilinganishwa na hospitali nyingine.
Naye
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo,
alisema wajawazito kati ya 50 hadi 80 wanajifungua hospitalini hapo kila
siku, 10 kati yao wakijifungua kwa njia ya upasuaji.
Dk
Mwabulambo alisema ipo haja kwa sekta binafsi kushirikiana na Serikali
ili kufanikisha mahitaji ya hospitali hiyo katika kuwahudumia wajawazito
na watoto.
No comments:
Post a Comment