.Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari,wengine pichani ni Maofisa waandamizi wa kampuni hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin akiongea na waandishi wa habari mjini Mwanza
Waandishi wa habari wakipata maelekezo mbalimbali walipotembelea kiwanda cha TBL Mwanza
Waandishi wa habari wakipata maelekezo mbalimbali walipotembelea kiwanda cha TBL Mwanza
Waandishi wa habari wakipata maelekezo mbalimbali walipotembelea kiwanda cha TBL Mwanza
Yawekeza zaidi ya shilingi bilioni 27/- katika sekta ya kilimo
Mkurugenzi Mkuu wa TBL
Group,Roberto Jarrin,amesema kuwa mtazamo wa kuifanya Tanzania nchi ya
viwanda unawezekana kutekelezeka kwa vitendo na kuongeza kuwa kampuni
yake itaendeleza mkakati wake wa kuchangia kuleta mabadiliko nchini
Tanzania kwa kuchangia kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta mbalimbali
zinazohusiana na kampuni hiyo.
Akitoa mwelekeo wa utendaji wa
kampuni yake kwa waandishi wa habari jijini Mwanza mwishoni mwa wiki
alisema “Mbali na kampuni yetu kuchangia pato la serikali kwa kiasi cha
shilingi bilioni 384/- kwa njia ya kodi imekuwa ikiziwezesha sekta
nyinginezo inazoshirikiana nazo kibiashara kuanzia kwa wakulima wa
nafaka mbalimbali hadi kwa watumiaji wa mwisho wa bidhaa zetu.”
Alisema kampuni itawekeza zaidi
kiasi cha shilingi bilioni 27/- katika kuwezesha maelfu ya wakulima wa
mazao ya Shahiri,mtama na mahindi kuongeza mavuno kutokana na kulima kwa
njia za kisasa-Wakulima watapatiwa utaalamu wa kilimo,mbegu bora na
udhamini kupata mikopo ya kuendesha kiilimo cha kisasa kutoka kwenye
mabenki inaoshirikiana nayo ambayo ni CRDB,NMB na Bank Of Africa (BOA).
Jarrin alisema kampuni pia
imechochea kukua kwa sekta ya usafirishaji nchini na kunufaisha jamii
na kuchangia pato la serikali ambapo imetumia kiasi cha shilingi bilioni
150/-katika usafirishaji wa malighafi mbalimbali kutoka zinapozalishwa
hadi kwenye viwanda vake pia wamekuwa wanasafirisha bidhaa
zinazozalishwa na kampuni kutoka viwandani hadi kwa watumiaji wa bidhaa
hizo waliosambaa nchini kote.Mwaka wa fedha wa kampuni ya TBL Group
umeanza tarehe 1 Aprili mwaka huu na utaisha tarehe 30 ya mwezi Machi
mwaka ujao wa 2017.
Alisema kampuni itaendelea
kutekeleza mpango wa kilimo shirikishi na wakulima wanaozalisha mazao ya
Shahiri,Mtama , mahindi na Zabibu nchini ambayo inayatumia kama
malighafi kwa ajili ya viwanda vyake na itahakikisha wanapata mazao ya
ziada kwa ajili ya kuboresha maisha yao na watasaidiwa kuunganishwa na
masoko mazuri ya kuuza mazao ya ziada kutoka taasisi zinazonunua mazao
hususani nafaka kwa ajili ya kusaidia jamii zenye upungufu wa chakula
kama vile Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa.
Kilimo cha Shahiri kinawawezesha
wakulima zaidi ya 3,000 wanaoishi vijijini nchini kunufaika kwa
kujipatia kipato cha uhakika na maisha bora-Shahiri ikivunwa inasindikwa
na kuwa kimea,malighafi ambao inatumika kutengenezea vinywaji vya
bia-Shahiri inayozalishwa nchini inakidhi mahitaji ya viwanda 2 vya TBL
Group vilivyopo katika mikoa ya Arusha na Mwanza ,kwa viwanda vingine
inaagiza malighafi hiyo kutoka nje ya nchi.Kwa upande wa kilimo cha
zabibu,TDL kampuni tanzu ya TBL Group inaendelea kuwezesha wakulima wa
zao la zabibu mkoani Dodoma kupitia mpango wa kilimo shirikishi na hadi
sasa wakulima zaidi ya 700 kutoka vijiji vya Bihawana, Mpunguzi,,
Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala
wamenufaika na mpango huu .
Wakulima wadogo wadogo wa zabibu
kupitia mpango huu wanawezeshwa kupatiwa mafunzo ya kilimo yanayotolewa
kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti wa kilimo ya Makutupora
Viticulture Training and Research Center (MVTRC),pia kupitia mfuko
ujulikanao kama Konyagi Social Trust – Zabibu na Shule Kwanza watoto wa
wakulima waliopo kwenye mpango huu wanawezeshwa kulipiwa gharama za
kupata elimu ya msingi na sekondari hususani watoto wa kike ambao
wamekuwa wakiachwa nyuma katika jamii .
Mbali na kuongeza wigo wa ajira
kupitia sekta ya kilimo,kampuni ya TBL Group inaongoza kwa kulipa kodi
nchini ikiwa imechangia pato la serikali katika kipindi cha miaka 10
kwa kiasi cha shilingi trilioni 2.3/-“Kampuni yetu imechangia kuleta
maendeleo ya nchi ya Tanzania kwa njia ya kukusanya na kulipa kodi za
serikali na imekuwa ikitunukiwa tuzo kutoka taasisi mbalimbali mojawapo
ikiwa tuzo ya mlipa kodi bora kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA
baada ya kuongoza kwa kukusanya na kulipa kodi nchini katika kipindi
cha miaka 4 mfululizo”.Alisema Jarrin.
Aliongeza kuwa kampuni ya TBL
Group ambayo ni mfano wa ubinafsishaji ulioleta mafanikio nchini
inawekeza zaidi ya shilingi bilioni 150/-kwa ajili ya kuendeleza
viwanda vyake ili viendane na teknolojia zenye viwango vya kimataifa
sambamba na viwanda vilivyopo katika nchi zilizoendelea.
Jarrin alisema kampuni inavyo
viwanda 10 vilivyopo katika mikoa mbalimbali nchini viwanda vyake
vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza na Arusha ni miongoni
mwa viwanda bora vya kampuni mama ya SABMiller vilivyopo katika nchi
mbalimbali duniani.Viwanda vya TBL Mwanza na Mbeya ni miongoni mwa
viwanda vinavyoshikilia rekodi ya kuwa viwanda bora vya bia kwa nafasi
ya juu ya 10 na 15 duniani.
Alisema bia zinazozalishwa na
viwanda vya TBL Group zinatawala soko kwa asilimia 78% baadhi yake
zikiwa ni Safari, Kilimanjaro, Ndovu, Castle Lager na Castle Lite
.Kampuni pia imekuwa kinara wa kutengeneza vinywaji vikali na mvinyo
ambavyo navyo vinatamba katika soko kwa asilimia 73% baadhi yake vikiwa
ni – Konyagi, Valeur na Dodoma Wine – Pia kampuni inatengeneza pombe
za asili baadhi yake zikiwa ni aina ya – Chibuku and Nzagamba –ambazo
zinatamba katika soko la vinywaji vya asili kwa asilimia 8% .Utafiti
uliofanywa na kampuni ya kimataifa ya utafiti wa matumizi ya bidhaa kwa
walaji ya CanBack umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili unatawala
soko la vinywaji vyenye kilevi Tanzania kwa asilimia 50%
Jarrin Alisema kutokana na ripoti
ya utafiti huo wa kitaalamu,TBL Group imeboresha zaidi vinywaji vya
asili aina ya Chibuku na Nzagamba vinavyotengenezwa na viwanda vyake
vya DarBrew ambapo vinapatikana kwenye chupa za ukubwa wa aina
mbalimbali kuwawezesha wateja kuvipata katika mazingira ya usafi wakati
huohuo kulingana na uwezo wa vipato vyao.Kupitia vinywaji hivi kampuni
imeanzisha mpango unaojulikana kama ‘Chibuku Mamas’ wa kuwawezesha
wanawake kuviuza na kujipatia mapato ambapo mpaka kufikia sasa
umenufaisha wanawake zaidi ya 130 na wengine wanaendelea kujiunga.
Kuhusu mtazamo wake wa biashara za
vinywaji katika siku za usoni,Mkurugenzi huyo wa TBL Group alisema zipo
changamoto mbalimbali baadhi yake wananchi wengi kutokuwa na vipato
vikubwa vya kuwawezesha kumudu kununua bia ikizingatiwa kuwa idadi kubwa
ya watanzania wana vipato visivyozidi shilingi 5,000/-kwa
siku,changamoto nyingine aliibainisha kuwa ni kutorasimishwa kwa pombe
za asili ambazo zinashindana na vinywaji vilivyorasimishwa kwenye soko
pia kutokuwepo motisha za kuzalisha malighafi za kutengeneza vinywaji
kama vile kupatikana Shahiri ya kutosha.
Akitoa maoni yake kuhusu namna ya
kuendeleza sekta hii ili iweze kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi
wa taifa alisema ni kupunguza kodi mbalimbali kwenye vinywaji ikiwemo
kupunguza kodi kwenye malighafi zinazozalishwa nchini kama kwenye kimea
malighafi inayotumika kutengenezea bia inayozalishwa nchini ikiwemo
kurasimisha pombe za asili “Pamoja na changamoto hizi na nyinginezo
kampuni inaendeleza mkakati wa kuunga mkono jitihada za serikali ya
awamu ya tano kuifanya Tanzania nchi ya viwanda na tayari tumethibitisha
kuwa dhana hii inatekelezeka kwa kuwa na viwanda bora hapa
vinavyotambulika kimataifa”.Alisema Jarrin.
No comments:
Post a Comment