Mwanariadha siata kalinga
akipokea kikombe cha mshindi wa tatu kwa riadha wanawake kutoka kwa mkuu
wa Naibu Mkuu wa majeshi wa Uganda Luteni Generali Charles Angina
(Picha na Selemani Semunyu)
Mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania
Luteni Generali Venance mabeyo akisalimiana na wachezaji wa timu ya
Soka ya Tanzania wakati wa mchezo wa mwisho dhidi ya Rwanda Tanzania
ilifungwa bao 1-0 na kushika nafasi ya tatu( picha na Selemani Semunyu)
Viongozi waandamizi wa majeshi waliowakilisha wakati wa
sherehe za kufungwa mashindano ya EAC kwa majeshi kiali nchini Rwanda
kutoka kulia ni mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali akifuatiwa na Mkuu wa
majeshi wa Kenya Jenerali Samson Mwathethe(wa pili kulia),Mnadhimu mkuu
wa JWTZ Luteni Jenerali Venance Mabeyo (Wapili kushoto) na Naibu mkuu
wa majeshi wa Uganda Luteni Jenerali Charles Angina(picha na Selemani
Semunyu)
NA SELEMANI SEMUNYU JWTZ
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA
TANZANIA LIMEIBUKA NA VIKOMBE VITATU KATIKA MASHINDANO YA MAJESHI KWA
NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI YALIYOFANYIKIA KIGALI NCHINI RWANDA TANGU
AGOSTI TANO HADI AGOSTI 17.
JWTZ ILIYOKUWA NA TIMU TANO ZA
RIADHA,SOKA,KIKAPU,MPIRA WA MIKONO
NA MPIRA WA PETE IMEFANIKIWA KUCHUKUA
USHINDI WA KWANZA IKWA UPANDE WA MPIRA WA PETE HUKU IKISHIKA NAFASI YA
TATU KWA MPIRA WA MIGUU NA RIADHA.
KWA UPANDE WAKE WAWAKILISHI WA
TIMU HIZO ZA TANZANIA NASRA SULEIMAN AMBAYE PIA NI MCHEZAJI BORA WA
MPIRA WA PETE NA DAMAS MAKWAYA WALOIKUWA NA HAYA YA KUSEMA MARA BAADA
KUKABIDHIWA VIKOMBE HIVYO.
NAHODHA WA WA SOKA DAMAS MAKWAYA
ALISEMA KATIKA MCHEZO WA MWISHO WALIZIDIWA MBINU LAKINI WANAIMANAI
SAFARI IJAYO WATABORESHA ZAIDI KIKOSI NA KUWEZA KUFIKIA MALENGO YAO YA
KUWA MABINGWA NA SIO MSHINDI WA TATU.
NASRA SULEIMAN ALISEMA TUZO NA
KIKOMBE WALICHOPATA WALISTAHILI WATAJITAHIDI KATIKA MASHINDANO YAJAYO
KUWEZA KUKILINDA NA KUFANYA VYEMA ZAIDI KWA NAFASI ZA USHINDI WA
UFUNGAJI BORA NA HATA MLINZI BORA.
KWA UPANDE WA SOKA MSHINDI NI
KENYA AKIFUATIWA NA RWANDA AMBAO WALIKUTANA KATIKA MCHEZZO WA MWISHO NA
TANZANIA AMBAPO WALIIBUKA NA USHINDI WA BAO MOJA
No comments:
Post a Comment