
Paka hao weusi wamepoteza mechi zao mbili za kwanza chini ya meneja Moyes ambaye alichukua nafasi ya Sam Allardyce ambaye ni meneja mpya wa England msimu huu.
Moyes aliongeza: 'Sidhani naweza kuficha ukweli. Watu watabaki hoi kwa sababu wanamatumaini kwamba kila kitu kitabadilika kimiujiza-haiwezi kubadilika na haitabadilika.'

Kampeini za mwaka 2010-11 ndio mara ya mwisho ambapo klabu hiyo haikubadilisha meneja katika msimu huo.
Meneja Steve Bruce, Martin O'Neill, Paolo di Canio, Gus Poyet, Dick Advocaat na Allardyce wote wamewajibika kwa klabu hiyo kwa misimu mitano iliyopita.
No comments:
Post a Comment