Dar es Salaam. Chama cha Wananchi (CUF), kimekutana na kuanza kikao cha Kamati ya Utendaji hivi sasa kitachojadili mambo mbalimbali ikiwamo maandalizi ya mkutano mkuu wa kesho utakaofanikisha upatikanaji wa Mwenyekiti mpya.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo ameiambia FOFAMMEDIA leo asubuhi kuwa kikao hicho kinafanyika Dar es Salaam na kikiisha kitafuatiwa na Baraza Kuu la Chama.
“Baraza la kuu pia litajidili na kuyapitisha majina ya nafasi ya uenyekiti na makamu mwenyekiti.Ambao wote watatangazwa jioni ,” amesema Mketo.
Mgombea wa uenyekiti wa chama hicho atakayepatikana kesho ataziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba aliyejiudhuru mwaka jana.
No comments:
Post a Comment