TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA
WA KIPINDUPINDU NCHINI PAMOJA NA TAHADHARI YA UGONJWA WA HOMA YA ZIKA,
LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO Y
A JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 8 FEBRUARI 2016.
A JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 8 FEBRUARI 2016.
Na Tabu Mullah
Kuhusu ugonjwa wa kipindupindu,
huu ni mwendelezo wa taarifa ya wiki kwa umma, ya Mwenendo wa Ugonjwa
huu hapa nchini. Hadi kufikia tarehe 7 Februari 2016, jumla ya watu
15325 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 238 wamepoteza maisha kwa
ugonjwa huu.
Takwimu za Kuanzia tarehe 1 hadi 7
Februari 2016, zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa Walioripotiwa wiki
hii imepungua kutoka 459 ya wiki iliyoishia tarehe 31 Januari hadi 258 Ambapo ni sawa na punguzo la asilimia 44. Kuna vifo 5, sawa na idadi ya
vifo vilivyoripotiwa katika wiki iliyopita.
Jumla ya mikoa ambayo imeripoti
kuwa na wagonjwa ni 13 ambapo mkoa wa Mara ndio umeongoza kwa kuripoti
idadi kubwa zaidi ya wagonjwa ukilinganishwa na mikoa mingine, ukiwa na
wagonjwa 73 (Musoma Vijijini 33, Musoma mjini 5, Bunda 1, Butiama 13,
na Tarime Vijijini 21), ukifuatiwa na mkoa wa Mwanza (70)- (Ukerewe 21,
Nyamagana 24, Ilemela 8, Sengerema 5 na Buchosa 12). Mikoa mingine ni
pamoja na Simiyu (30), Morogoro (26) na Kilimanjaro (16).
Katika mapambano ya kudhibiti
mlipuko huu wa Kipindupindu, kuna changamoto mbalimbali zilizobainishwa
na Wizara yangu kupitia wataalam ambao wanashirikiana na timu zilizopo
katika mikoa na wilaya zilizoathirika. Mojawapo wa changamoto ni utoaji
wa idadi pungufu ya wagonjwa au kutotoa kabisa taarifa za wagonjwa wa
Kipindupindu. Hii inapelekea kusababisha mikakati iliyowekwa kutokuwa na
mafanikio hivyo ugonjwa kuendelea kuwa ni tishio katika jamii.
Ninapenda kusisitiza kuwa, taarifa za wagonjwa wa Kipindupindu zitolewe
bila kuficha, na watendaji watakaoficha taarifa za wagonjwa
watawajibishwa ipasavyo.
Changamoto nyingine iliyopo ni
ushiriki mdogo wa sekta nyingine katika kupambana na ugonjwa huu.
Ninaomba ieleweke kuwa mapambano dhidi ya Kipindupindu yatafanikiwa
ikiwa sekta nyingine kama Maji, miundombinu, biashara, elimu, mazingira
n.k zitashirikiana. Wizara yangu imeendelea kusisitiiza ushirikiano huu
katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya, ili mipango ya kupambana na
Kipindupindu ishirikishe sekta mbalimbali na pia Mashirika yasiyo ya
Kiserikali, Taasisi za Dini na Vyombo ya Habari.
KAMATI KUU YAFANYA UTEUZI WA WAGOMBEA WATAKAOZIBA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI CC
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Mhe. Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari
katika ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM, Ofisi Ndogo Lumumba.
Jana tarehe 07/02/2016 Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilikuwa na kikao maalum cha siku moja mjini
Dodoma. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete. Kikao hicho kilikuwa na kazi ya kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali
zilizo wazi za uongozi ndani ya CCM mikoani na wilayani ambazo uteuzi wake upo
kwenye Mamlaka ya Vikao vya Chama Taifa.
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilikuwa na kikao maalum cha siku moja mjini
Dodoma. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete. Kikao hicho kilikuwa na kazi ya kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali
zilizo wazi za uongozi ndani ya CCM mikoani na wilayani ambazo uteuzi wake upo
kwenye Mamlaka ya Vikao vya Chama Taifa.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YAANZA KAZI RASMI – YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHINI
- Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad
Masauni akijitambulisha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kabla ya Kamati hiyo kuipokea taarifa ya
Wizara hiyo katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo baada ya kuundwa na
Bunge hivi karibuni. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Balozi Adadi Mohamed Rajabu anayefuatia ni Makamu wake, Kanali Masoud
Khamis. Kulia kwa Masauni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali
Projest Rwegasira. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo.
- Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Mohamed Rajabu akizungumza jambo na Wajumbe wa Kamati yake pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kikao chao kwanza tangu Kamati hiyo iundwe na Bunge hivi karibuni. Wapili kulia mstari wa mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni, na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kanali Masoud Khamis. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo.
- Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad
Masauni akitoa taarifa ya Wizara katika kikao cha kwanza cha Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kikao hicho
kilichohudhuriwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Maafisa wa Wizara,
kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar
es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi M
No comments:
Post a Comment