Tuesday 16 February 2016

Hatua Mbalimbali zilizofikiwa Ujenzi wa Barabara ya Morocco kwenda Mwenge

MOR1
Sehemu ya  Barabara ya Morocco kwenda Mwenge ikiwa katika  hatua  ya kutolewa tabaka ya Udongo wa  chini na kuwekwa tabaka ya udongo mpya kama inavyooenekana katika picha leo jijini Dar es Salaam .
MOR2
Mafundi  kutoka kampuni ya Ujenzi  ya  ESTIM wakiwa kazini katika hatua ya kutoa udongo wa chini  kwa ajili ya kuweka udongo mpya  ,ambapo ujnzi huo unatarajiwa kumalika mapema Mei mwaka huu.
MOR3 MOR4
Kipande cha Barabara ya Mwenge-Morocco kilicho kamilika kwa kiwango cha lami katika eneo la Mwenge-Bamaga kinavyoonekana katika picha . (Picha na Lorietha Laurence –Maelezo).
MOR5
Mafundi wakijengea bomba la maji eneo la Makumbusho  kwa kuliwekea zege na nondo   ili kulihakikishia  usalama wake wakati wa ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco inayotarajiwa kukamilika mapema mwezi Mei mwaka huu.
MOR6
Mafundi wakijengea bomba la maji eneo la Makumbusho  kwa kuliwekea zege na nondo   ili kulihakikishia  usalama wake wakati wa ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco inayotarajiwa kukamilika mapema mwezi Mei mwaka huu.
MOR7
Afisa Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Bi.Aisha Malima akipata maelezo kutoka kwa Fundi Mchundo (Civil Technician) wa Kampuni ya Ujenzi  ya ESTIM ,Bw. Kano Warema  kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco leo jijini Dar es Salaam.

IGP Akiwaapisha  Makamishna Wa  Polisi Waliopandishwa Vyeo  Na Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli

KUA1
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu akimuapisha Kamishna wa Polisi, CP Simon Sirro baada ya kupandishwa cheo  na Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,  kutoka Naibu Kamishna wa Polisi na kuwa Kamishna wa Polisi ambapo pia amemteua kuwa Kamanda  wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
KUA2
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu akimuapisha Kamishna wa Polisi, CP Albert Nyamuhanga  baada ya kupandishwa cheo  na Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,  kutoka Naibu Kamishna wa Polisi na kuwa Kamishna wa Polisi ambapo pia amemteua kuwa Kamishna wa Fedha na Logostiki wa Jeshi la Polisi.
KUA3
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu akimuapisha Kamishna wa Polisi, CP Robert Boaz baada ya kupandishwa cheo  na Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri wa Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,  kutoka Naibu Kamishna wa Polisi na kuwa Kamishna wa Polisi ambapo pia amemteua kuwa Kamishna wa Intelijensia wa Jeshi la Polisi.
KUA4
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu akimuapisha Kamishna wa Polisi, CP Nsato Marijani baada ya kupandishwa cheo  na Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,  kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi na kuwa Kamishna wa Polisi ambapo pia amemteua kuwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi.
KUA5
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu (kushoto) akimpongeza Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Nsato  Marijani baada ya kumuapisha jana Makao makuu ya Jeshi la Polisi. CP Nsato Marijani amepandishwa cheo na Mheshimiwa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi na kuwa Kamishna wa Polisi ambapo pia amemteua kuwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment