Wednesday 17 February 2016

Mayanja Ntaifunga Yanga Bao 3-0





Kocha Jackson Mayanja wa Simba SC amesema anaweza kuwafunga Yanga SC Hata 3-0

sitaki kuonekana kwamba ninaleta maneno mengi, bali ninachokueleza ndiyo Ukweli. Nimeisoma mifumo anayoitumia Pluijm Yanga na nimejaribu kutafuta Mbinu za kutegua mbinu zake anazotumia. Pluijm kwenye michezo mingi Amekuwa akitumia mfumo wa 4-3-3, ambao ni mfumo unaohitaji washambuliaji Watatu wenye kuweza kucheza kitimu, lazima wawe na uwezo binafsi Utakaowawezesha kuibeba timu inapozidiwa,”amesema kocha huyo wa zamani Wa Kagera Sugar. 

Mayanja ambaye enzi zake alichezea SC Villa na KCCA za kwao Uganda, Amesema hana uhakika kama washambuliaji watatu wa Yanga SC, Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma, Amissi Joselyn Tambwe na Simon Happygod Msuva Wanaweza kucheza mfumo huo ipasavayo. “Kama amekuwa akipata matokeo (mazuri) kwa mfumo huo, basi ni dhidi ya timu dhaifu na siyo Simba yangu,” Amesema.

“Bila kuwa na mfumo unaoendana na wachezaji wako ni kazi bure, kama Yanga Wakiamua kutumia mifumo ambayo wamekuwa wakiitumia siku zote, basi kwangu Nafakiri itakuwa sherehe. Ninaweza kutamba mapema nitawafunga hata mabao 3-0,” amesema. 

Watani wa jadi, Simba SC na Yanga wanatarajiwa kukutana Jumamosi katika Mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa marudiano.

Mchezo wa kwanza Septemba 26, mwaka jana mabao ya Amissi Tambwe kipindi cha kwanza na Malimi Busungu kipindi cha pili yalitosha kuipa Yanga ushindi wa 2-0 dhdii ya watani wao hao wa jadi Uwanja wa Taifa.
Simba SC imeweka kambi mjini Morogoro, wakati Yanga SC wapo kisiwani Pemba kwa maandalizi ya mchezo huo

No comments:

Post a Comment