Tuesday 23 February 2016

Halmashauri ya Wilaya YA Kinondoni Yapanga Kununu Magari 40 ya kukusanya Taka Ngumu

SAM_1212
Na Kalonga Kasati
HALMASHAURI Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam katika mwaka kipindi cha 2016/17 imepanga kununua magari 40 yatakayotumika kwa ajili ya zoezi la ukusanyaji wa taka ngumu katika Kata na Mitaa ya Halmashauri hiyo.

Hatua inaelezwa itasaidia kuondoa kero ya mlindukano wa taka ngumu ambazo huzagaa ovyo, kutokana na hushindwa kukusanywa kwa wakati na makampuni ya wakandarasi wa usafi katika Kata na Mitaa wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza na MAELEZO leo (Jumanne Februari 23, 2016), Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Sebastian Mhowera alisema tayari ofisi hiyo pamoja na Halmashauri za Wilaya ya Ilala na Temeke zimewasilisha ombi maalum la kuomba kibali cha ununuzi wa magari hayo katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Kwa mujibu wa Mhowera alisema Halmashauri hiyo huzalisha jumla tani 2020 za taka ngumu ambapo uwezo uliopo ni kuteketeza tani 1300 kwa siku, na hivyo kiasi kinachobaki huibua changamoto katika namna ya kukabiliana na ongezeko hilo.

“Kiasi kikubwa cha taka zinazozalishwa nyingi hubakia mitaani na hazifiki barabarani ambapo ndipo hukusanywa kwa ajili ya kupelekwa dampo, kwani vitendea kazi katika maeneo hayo ni changamoto” alisema Mhowera.

Alisema kwa mujibu wa Sera ya Usafi, Makampuni ya Wakandarasi wa Usafi yaliyopo katika Mitaa yana wajibu wa kukusanya taka zote kwani husimamiwa na wananchi wenyewe, ambapo hata hivyo makandarasi mengi yamekuwa hayana uwezo wa kufanya kazi hiyo.

Aidha Mhowera alisema katika kufanikisha zoezi la usafi wa mazingira linalofanyika kila mwisho wa mwezi nchini, Halamshauri hiyo imetoa maelezo mbalimbali ya kiutendaji kwa Maaafisa Watendaji wa Mitaa na Kata.

No comments:

Post a Comment