Wednesday 24 February 2016

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi katibu Mkuu Wamekula Viapo vya kuingoza Tume ya Utumishi ya Jeshi la polisi na Magereza

mas1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akila kiapo cha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mas2
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akila kiapo cha kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mas3
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni  mara baada ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mas4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment