Sunday 28 February 2016

Kapombe Mchezaji Bora Mwezi Januari 2016

x2-kdg


Na Tabu Mullah
Beki Shomari Kapombe wa timu ya Azam FC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Januari 2016.
Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Kapombe alicheza dakika zote 180 za mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo Shooting. Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons ilikuwa kiporo, na ilichezwa Februari24, 2016.
Kapombe alifunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 wa timu yake dhidi ya Mgambo Shooting. Pia alisaidia kupatikana bao la Azam kwenye mechi dhidi ya African Sports iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, na mara nyingi mashambulizi ya timu yake yalianzia upande wake.
Washindani wa Kapombe kwenye kinyang’anyiro hicho katika mwezi huo walikuwa mshambuliaji wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Jeremiah Juma na beki wa Coastal Union ya Tanga, Miraji Adam.
Kwa kutwaa tuzo hiyo, Kapombe atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Limited.

FULL MKANDA PAMBANO LA CHEKA NA MSERBIA LEADERS JANA, CHEKA ASHINDA KWA …’.POINTI’

 Bondia Mtanzania Francis Cheka (kulia) akichapana na mpinzani wake bondia kutoka nchini Serbia, Geard Ajetovic, wakati wa pambano lao la raundi 12 la ubingwa wa Mabara , uzito wa Super Midle wa WBF lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 
Katika raundi ya kwanza bondia Cheka alionekana kuanza kwa woga na kumfanya mpinzani wake kumshambilia kwa ngumi za kushitukiza na kumpeleka chini, jambo lililomfanya Cheka kuchanganyikiwa na kuhesabiwa na mwamuzi na kisha kuendelea na pambano.
 
Baada ya kwenda chini katika raundi ya kwanza raundi ya pili cheka alionekana kucheza kwa tahadhari kubwa kwa kupiga na kukimbia huku mpinzani wake akionekana kujigadi muda wote na kupiga ngumi za kushitukiza zilizokuwa na madhara kwa Cheka.
Katika pambano hilo Bondia Francs Cheka, aliibuka na ushindi kwa pointi
 Cheka akijitahidi kupangua konde la mpinzani wake….
 Cheka, alichanika katika raundi ya nane baada ya mpinzani wake kumbananisha kwenye kona iliyokuwa na utelezi ambapo aliteleza na kupoteza mwelekeo na kushambuliwa mfululizo. Na Mafoto Blog.

No comments:

Post a Comment