Thursday 25 February 2016

KAMPUNI YA KUOSHA MAGARI KWA KUTUMIA MVUKE YA SHINE ECO WASH LIMITED YATUA JIJINI DAR ES SALAAM

AD1
Baadhi ya magari ya wateja yakiendelea kuoshwa katika kampuni ya Shine Eco Wash Limited yenye makazi yake Mlimani City jijini Dar es Salaam.
AD2
Mmoja wa wafanyakazi katika kampuni ya Shine Eco Wash Limited yenye makazi yake Mlimani City jijini Dar es Salaam akiendelea na kazi ya uoshaji.
AD3
Kazi ya uoshaji wa magari ikiendelea katika kampuni hiyo
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Tabu Mullah
Kampuni inayojishughulisha na uoshaji wa magari kwa njia ya mvuke imeanza kutoa huduma zake jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahojiano maalum Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Elia  Richard Moshi alisema kuwa lengo la  kampuni hiyo ni  kutoa  huduma ya kipekee kwa kuosha magari kwa kutumia mvuke ni kuzuia uharibifu wa mazingira.

Akielezea utofauti wa huduma hiyo na huduma zingine Moshi alisema kuwa kampuni inatumia maji yasiyo na kemikali ya aina yoyote (distilled water) ambapo  gari moja  huoshwa kwa  kutumia lita tatu hadi  tano za maji kwa njia  ya mvuke ijulikanayo kama steaming.

Alisema kuwa  awali alifanya  utafiti na kubaini  kuwa kwa kawaida gari moja  huoshwa kwa kutumia  lita 85 hadi 125 hali inayochochea upotevu wa maji na uharibifu wa mazingira, hali iliyopelekea yeye  kubuni  wazo la kuanzisha kampuni ya kuosha magari kwa kutumia maji kidogo yasiyo na kemikali kwa kutumia mashine maaluum.

Aliongeza kuwa huduma nyingine wanazotoa kama kampuni ni pamoja na kung’arisha magari kwa nje (body polishing) ili kuondoa mikwaruzo na madoa sugu, kung’arisha  gari kwa ndani  (interior polishing) na kusafisha  engine bila kutumia  maji.

“Unajua unapotumia maji kuosha  engine ya gari  hususan kwa magari ya kisasa, unaharibu  gari, hivyo  tunaosha  bila kutumia maji  kwa kutumia mashine maalum  pamoja na kung’arisha,”alifafanua Moshi.

Aliendelea kufafanua kuwa watumiaji wa magari wanashauriwa kuosha magari   kwa kutumia mvuke angalau mara moja kwa mwezi na kuwataka wamiliki wote waishio jijini Dar es salaam kupeleka  magari yao katika  kampuni yake  yenye  makazi yake katika  viwanja  vya Mlimani City kwa ajili ya kuoshwa.

Akielezea malengo ya kampuni yake katika kusambaza huduma kwa wafanyakazi waliopo maofisini, Moshi alisema kuwa kampuni ina mashine maalum (mobile machine) zenye uwezo wa kufanya kazi sehemu yoyote ambapo wateja wanaweza kusogezewa huduma  kwenye maofisi yao.
“Wateja waliopo maofisini wana uwezo wa kujiorodhesha na sisi kama kampuni kuwafuata maofisini  na kuwaoshea magari yao kwenye parking zao  huku wakiendelea na shughuli zao kama kawaida na kwa usalama zaidi” alifafanua.

Hata hivyo aliongeza kuwa kampuni ina mpango wa kufungua matawi jijini Dar es Salaam na katika mikoa ya Arusha, Dodoma na Kilimanjaro na mingine kwa siku za usoni
Wakizungumza kwa nyakati  tofauti wakazi wa jijini  Dar es Salaam kuhusu  huduma ya kampuni hiyo walisema kuwa wameanza kunufaika na huduma hiyo na kufurahishwa na utendaji kazi wa kampuni hiyo.

Salum Salehe mkazi wa Masaki jijini Dar es salaam alisema kuwa  tangu ameanza kutumia huduma hiyo, gari yake imekuwa ikionekana mpya kila  kukicha na kuwataka watumiaji wengine  wa magari kutumia kampuni hiyo katika uoshaji wa magari yao.

Alisema kuwa mbali na mwonekano wa gari yake kuimarika, kampuni hiyo imekuwa ikokoa muda mwingi kwani anakabidhi gari kwa kampuni na kuendelea na majukumu yake kama kawaida ambapo hufuata baadaye baada ya kazi ya uoshaji kukamilika.
Naye Victor Moshi mkazi wa Kinondoni aliongeza kuwa  kampuni hiyo  imekuwa ikiwasiliana na wateja wake  kwa njia ya sms kwa ajili ya kuwashauri  juu ya utunzaji wa magari yao jambo ambalo ni jema.

WIZARA YALAANI MAUAJI YA MTOTO MARIAM DEOGRATIUS (4) ALIYEBAKWA NA KUUAWA ENEO LA MAKOKO, MUSOMA MKOANI MARA

download (2)
Wizara inalaani vikali tukio la kubakwa na kuuawa kikatili kwa mtoto Mariam Deoratius, umri miaka 4, ambaye alifanyiwa ukatili huo na watu wasiojulikana, eneo la Makoko, Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, mapema wiki hii. 

Wizara imesikitishwa na mazingira ya mauaji ya mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia, ambaye aliokotwa kwenye banda linalojengwa akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri, kutokwa na damu nyingi na akiwa amefariki dunia. Mauaji haya ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi ya mtoto ambayo ndiyo ni haki yake ya msingi. Haki hii inapovunjwa inarudisha nyuma jitihada za Taifa letu kufanya jamii zetu kuwa mahali salama kwa watoto kuishi.

Wizara inaamini kuwa, Mamlaka zinazohusika na ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili katika Mkoa wa Mara hususan Manispaa ya Musoma, kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka, na kuwa
fundisho kwa wanaoendeleza ukatili wa watoto. Kwa tukio hili, jamii inahimizwa kubadilika na kuhakikisha kuwa ulinzi wa watoto ni jukumu la wazazi, walezi na watu wote katika jamii.
Wizara inatoa pole kwa wazazi, ndugu, marafiki na familia ya mtoto Mariam aliyeuawa katika umri mdogo na tunawaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
  1. S.  Nkinga
              KATIBU MKUU
               25/02/2016

No comments:

Post a Comment