Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe
(hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa
Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay,
jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa
Wizara hiyo, Marlin Komba. Kulia ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA),
Esaka Mugasa. Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki
silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya
operesheni ya kuwakamata haijaanza.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba akizungumza na wajumbe
(hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa
Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay,
jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu ili aweze
kuifungua warsha hiyo ya siku mbili.
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA),
Esaka Mugasa akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya
Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa
Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Watatu
kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa
Wizara hiyo, Marlin Komba. Katibu Mkuu katika hotuba yake ya ufunguzi
wa warsha hiyo, aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali
kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kulia) akitoka
katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es
Salaam mara baada ya kufungua Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya
Udhibiti wa Silaha na Risasi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria
wa Wizara hiyo, Marlin Komba, wapili kushoto ni Naibu Kamishna wa Jeshi
la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi na kulia ni Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe
wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi
katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es
Salaam. Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki
silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya
operesheni ya kuwakamata haijaanza
Sehemu ya wajumbe wa Warsha ya
Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi wakimsikiliza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe hao
katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es
Salaam kabla ya kuwafungulia warsha yao ya siku mbili itakayojadili
umasishaji wa Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha ya Mwaka 2015. Hata
hivyo, katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha
nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya
operesheni ya kuwakamata haijaanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati waliokaa),
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba (wapili
kushoto waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron
Gyimbi (wapili kulia), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP),
Yusuph Ilembo (kulia) na kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA),
Esaka Mugasa, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya
Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Warsha hiyo ya
siku mbili ilifunguliwa na Katibu Mkuu, Rwegasira katika Ukumbi wa Bwalo
la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
WAKAZI WA RUFIJI MKOANI PWANI WAKUMBWA NA MAFURIKO WAKOSA SEHEMU YA KUISHI
Na Tabu Mullah
WANANCHI zaidi ya 5000 katika
Wilaya ya rufiki Mkaoani Pwani kwa sasa hawana mahali pakuishi kutokana
na nyumba zao kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Kufuatia kutokea kwa mafuriko
hayo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injiania Evarist Ndikilo amekwenda katika
eneo la tukio na kujionea athari zilizojitokeza kwa wananachi hao wa
wilyani rufiji kutokana na mvua hizo zilizosaababisha mafuriko.
Akizungumza na wahanga wa
mafuriko hayo Ndikio alisema kwamba kutokana na hai hiyo serikali Mkoa
wa Pwani imechukua hatua za haraka kuwasaidia wananci hao kwa kutoa
chakula cha dharura tani 1283 za mahindi kwa ajili ya wananchi hao.
Ndikilo alisema kuwa mbali na
serikali kutoa tani hizo za mahindi pia imetoa mbegu za mahindi tani 10
sambamba na tani 5 za mtama ambazo zinastawi kwa kipindi cha mudamfupi
ii wannaachi waweze kuzipanda katika ukanda wa juu ii ziweze kuwasaidia
katika upatikanaji wa chakula.
“Kwanza kabisa mimi nawapa pole
wale wote ambao wamepata na maafa haya ya mafuriko na wengine kukosa
sehemu ya kuishi lakini nataka kuwahakikishia kuwa serikali yenu ipo
pamoja nanyi katika kuhakikisha unawasaidia huduma zote muhimu ambazo
zinastaili ikiwemo kuwapatia chakula kw ahiyo msiwe na hofu yoyote,”
“Lakini ombi langu kubwa kwa
kipindi hiki kwa wanaanchi ni kuwa makini sana kwani mvua bado
zinaendelea kunyesha na na zimeleta maafa makubwa kama mnavyoona kwa
hiyo cha msingi kama kuwa wnanchi bado wanaendelea na shughuli za kulima
karibu na mabonde ya mito wasiendelee kulima katika maeneo hayo kwani
wanaweza kusombwa na maji,”alifafanua Ndikilo.
Pia Ndikio aliwaomba wahanga
hao wa mafuriko kuhakikisha wanakitumia vizuri chakula amabcho
kimetolewa na serikali kwani katika kipindi hiki uende mahitaji ya
chakula yakaongezeka zaidi kutokana na mahitaji mwengi ya wananchi
wenywe hivyo ni vema kuwa na matumizi mazuri.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa sasa kazi kubwa inayofanywa na serikali ni kutoa elimu kwa wananachi na kuwahamasisha wale wote waliokumbwa na mafuriko watoke mara moja katika maeneo ya mashamba kwani ni hatari kwa masiha yao pindi mvua inaponyesha.
Akizungumzia kuhusina na baadhi ya wafanyabiashara amabo
wamekuwa na tabia ya kupandisha bei ya vyakula pindi wnapoona maafa kama
hayo yamejitokeza waacha mara moja kufanya hivyo kwani ni kwakandamiza
wananchi.
” Wafanyabiashara
wasiowaungwana wasitumie janga hili kujinufaisha kwa kupandisha bei ya
vyakula, kwa kutambua hilo tumewapa vibali wafanyabishara 6 wenye uwezo
ili wanunue tan 10 za mahindi na kusaga unga na kuwauzia wananchi kwa
bei nafuu kwa jimbo la kibiti na ikwiriri,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Rufiji Nurdin Babu aibainisha kuwa kutoka ana mvua hizo zinazoendelea kunyesha tayari jumla ya hekta 8138.4 za mpunga na tani 7171.2 za mahindi zimeathirika na maji na kuwa mazao hayo yalikuwa katika hatua za mwisho kwa ajii ya kuvunwa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Rufiji Nurdin Babu aibainisha kuwa kutoka ana mvua hizo zinazoendelea kunyesha tayari jumla ya hekta 8138.4 za mpunga na tani 7171.2 za mahindi zimeathirika na maji na kuwa mazao hayo yalikuwa katika hatua za mwisho kwa ajii ya kuvunwa.
Babu aliongeza mafuriko
yaliyotokea katika wilaya yake yalianza tangu juzi usiku na kuvikumba
vijiji mbali mbali ikiwemo kijiji cha uwe na mhoro na kusababisha
daraja la muhoro kuvunjika na hivyo wananchi kuvuka kwa kutumia mitumbwi
pamoja na boti.
Rais Magufuli ampa pole mke wa Waziri mkuu Mstaafu mama Tunu Pinda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa
Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari,
iliyotokea jana tarehe 08 Februai, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma
kwenda Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea katika eneo
la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa
akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha
pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.
Katika salamu hizo alizozituma
kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda,
Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali
hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.
“Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri
Mkuu Mstaafu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda
kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye
majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku” alisema
Rais Magufuli.
Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment