Tuesday 16 February 2016

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amepongeza Jitihada zinazofanywa na watafiti kwa kurudisha Mbwa Mwitu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti

MAG2Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) katika tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
MAG3
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe  (MB) akiongeawakati wa  tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
MAG4Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe  (MB) akielekea katika boma la mbwa mwitu kwa ajili ya tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
MAG5Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe  (MB) akikata utepe kuruhusu kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kutoka nje kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
MAG6Wanahabari wakichukua picha mbalimbali wakati mbwa mwitu walipokuwa wakitoka kwenye boma.
MAG7Kundi la sita la mbwa mwitu 11 wakitoka katika boma maalum katika Hifadhi ya Serengeti.
MAG9Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi akiongea na wanahabari mara baada ya tukio la kuachiwa kwa mbwa mwitu.
MAG11Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiwa katika picha ya pamoja na askari wa  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amepongeza jitihada zinazofanywa na watafiti kwa kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti baada ya kutoweka katika miaka ya tisini. Waziri Maghembe alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipokuwa akiachia huru kundi la sita la mbwa 17 waliokuwa wamehifadhiwa katika boma maalum ili kurejea katika makazi yao ya asili.
Profesa Maghembe amesema serikali itaendelea kuwekeza katika eneo la utafiti ili kuwezesha sekta ya uhifadhi nchini kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. Alisema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sekta nyingi ikiwemo ya uhifadhi na kuwa wanyama wamekuwa wakiathirika na mabadiliko hayo hivyo ni vema uwekezaji mkubwa ukafanyika katika eneo la utafiti ili kujua namna ambavyo uhifadhi unaweza kukabiliana na mabadiliko hayo.
Mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu unalenga kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambao walitoweka kabisa tangu mwaka 1994 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaweza kubainika kisayansi. Mradi huu unasimamiwa na kuendeshwa na watafiti wa kitanzania.
Tangu kuanza kwa mradi huu mwaka 2011, jumla ya makundi sita ya mbwa mwitu wamesharudishwa ndani ya Hifadhi ya Serengeti. Makundi haya ni pamoja na Vodacom ambapo Kampuni hii ya simu ilifadhili gharama za mradi; Serengeti; Loliondo; Kikwete; Nyasirori na hili la mwisho ambalo lilipewa jina la Markus Borner, mwanasayansi kutoka nchini Ujerumani aliyetumia miaka 35 akifanya shughuli za uhifadhi katika hifadhi ya Serengeti.
Mradi wa mbwa mwitu Serengeti unaendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, TANAPA na Chuo Kikuu cha Glasgow.

Katibu Mkuu Mambo  Ya  Ndani  Ya  Nchi Atembelea Vituo Vya  Uhamiaji Vya Mipakani  Mkoa Wa Kilimanjaro

UH1
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Tarakea, wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, John Kapembe akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) eneo la Tanzania katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya. Rwegasira yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akitembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani humo.
UH2
Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kulia) wakati alipowasili katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha huduma mpakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea mipaka ya Uhamiaji mkoani humo Watatu kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
UH3
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) azungumze na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Rwegasira aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.
UH4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) akizungumza na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Meja Jenerali Rwegasira katika hotuba yake aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.
UH5
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Holili, Edwin Mwasota akimuonyesha  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (watatu kulia) moja ya ofisi zilizopo katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Meja Jenerali Rwegasira alifanya ziara ya kikazi kwa kutembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani Kilimanjaro.
UH6
Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku (kushoto) akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto) mpaka Tanzania pamoja na Jengo la Uhamiaji la nchini Kenya (Taveta) wakati walipokuwa juu ya ghorofa ya Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro.
UH7
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) akiondoka katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumaliza ziara yake ya kulitembelea jengo hilo na kuzungumza na maafisa mbalimbali wa serikali wanaotoa huduma za mpakani mkoani humo. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku na Kulia ni Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpakani Holili, Aden Mwakalobo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri  Mbarawa Asisitiza Ukusanyaji  Wa  Mapato Katika Sekta Ya  Miundombinu.

PR1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na mkandarasi Nyanza Road Works anayejenga barabara ya Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51. (Wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bw. Joshua Mirumbe.
PR2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisolya kuhusu ujenzi wa mradi wa barabara ya Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
PR3
Muonekano wa barabara ya Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambayo ni sehemu ya barabara ya Nyamuswa-Bunda hadi Nansio Km 121.9.
PR4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Emmanuel Koroso (wa pili kulia) wakati akikagua daraja la Kyarano linalounganisha barabara ya Makutano-Nata- Mto wa Mbu yenye urefu wa Km 467.7.
PR5
Muonekano wa daraja la Kyarano linalounganisha barabara ya Makutano-Nata- Mto wa Mbu yenye urefu wa Km 467.7 likiwa katika hatua za ujenzi.
PR6
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na watumishi wa sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (hawapo pichani) kuhusu kufanya kazi kwa umoja na kuongeza mapato katika sekta zao,  mkoani Mara.
PR7
Meneja wa uwanja wa ndege wa Musoma Bi. Bertha Bankwa akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika mkutano wa watumishi wa sekta zilizo chini ya Wizara hiyo.
PR8
Daraja la reli linaloingia baharini katika bandari ya Musoma kupokea na kupakia mizigo kwenye melikwa ajili ya kuisafirisha katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Na Yahya Njenge

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka watendaji walio chini ya Wizara yake kuongeza kasi ya kukusanya mapato ili kuwezesha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi kufikiwa kwa wakati.

Akizungumza na watumishi wa sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino mjini Musoma, Prof. Makame Mbarawa amesema kufanya kazi kwa umoja, uadilifu, uwazi na ubunifu kutasababisha kufikiwa kwa malengo hayo mapema.

“Kama mtu hawezi kufanya kazi kwa kasi na kwa malengo yanayotekelezeka na kupimika Atupishe kabla hatujamuondoa, hatuta muonea mtu na hatutamvumilia mtu atakayeshindwa kuendana na kasi yetu”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema Serikali imetenga zaidi ya dola milioni 30 kwa ajili ya kukarabati Uwanja wa ndege wa Musoma na kununua magari ya kisasa ya zimamoto ili kurudisha hadhi ya uwanja huo.
Aidha, amezitaka taasisi za Serikali zinazodaiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mkoani Mara kulipa madeni yao ili kuuwezesha wakala huo kufanya kazi kwa kasi na kufikia malengo yaliyowekwa.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Makutano-Nata-Mto wa Mbu yenye urefu wa km 467.7 inayojengwa na makandarasi wazalendo kumi na kutaka Mkandarasi anayejenga kipande cha km50 kutoka Makutano hadi Sanzate kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa haraka ikiwemo daraja la kyarano ili kuiwezesha barabara hiyo kupitika wakati wote wa mwaka.

Amemwagiza Meneja Wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa Mara Eng. Emmanuel Koroso kuhakikisha makandarasi wanaojenga barabara mkoani humo wanarejea kazini  kwa kuwa serikali imeanza kulipa madai yao.

Ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kutumia fedha zilizotumwa kutoka Mfuko wa Barabara (RFB) kutumika kwa miradi iliyokusudiwa ili kuingunisha wilaya hiyo mpya na wilaya nyingine mkoani Mara kwa barabara za lami.

Akiwa wilayani Bunda Prof. Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works anayejenga Barabara ya Buliamba-Kisolya Km 51 kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo kwa mujibu wa Mkataba kwani serikali imeshalipa fedha shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisolya-Nansio yenye urefu wa Km 121.9.

Aidha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa amewataka viongozi wa Wilaya za Magu, Bunda na Musoma kufanya kampeni kubwa ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulinda Miundombinu ya Barabara, Reli na Mkongo wa taifa wa Mawasiliano ili isihujumiwe na kusababisha usumbufu kwa jamii na kuisababishia serikali hasara.

Naye, Mbunge wa Mwibara Mhe. Kangi Lugola amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa kukamilika kwa barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisolya hadi Nansio yenye urefu wa KM 121.9 itasaidia kukuza uchumi wa Wilaya ya Bunda na Ukerewe kwa kuwa eneo hilo lina shughuli nyingi za uchumi zinazotokana na kilimo, ufugaji na uvuvi wa Samaki.

Prof. Mbarawa amewataka makandarasi wote nchini kuhakikisha wanawapa wafanyakazi wao mikataba kulingana na sheria za nchi ili kuwezesha miradi ya barabara inayoendelea kujengwa kukamilika kwa wakati na kuondokana na hujuma zinazoweza kudhoofisha ujenzi wa barabara na miundombinu mingine.

“Lindeni miundombinu ili idumu kwa muda mrefu, barabara, reli na mkongo wa taifa ni Miongoni mwa miundombinu inayojengwa kwa fedha nyingi na kuhujumiwa mara kwa mara hivyo kuisababishia Serikali hasara”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa yupo kwenye ziara ya kukagua Ujenzi wa miundombinu ya barabara, Bandari na mkongo wa taifa wa mawasiliano katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo Ametembelea Wilaya za Magu, Bunda, Butiama na Musoma.

No comments:

Post a Comment