Wednesday 24 February 2016

Ridhiwani na Diwani wa Vigwaza Wagomea kupokea Mradi wa Maji

images (8)
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete ameungana na wakazi wa vijiji vitatu vya Kidogozelo,Kitonga na Milo,kata ya Vigwaza ,kukataa kukabidhiwa mradi wa maji uliogharimu kiasi cha sh.Mil 258 fedha kutoka bank ya dunia .

Mradi huo umekataliwa kutokana na kutokamilika pamoja na kuonekana mapungufu makubwa ikiwa ni pamoja na mabomba kuwekwa karibu na ardhi,kupasuka kabla ya matumizi na kutandazwa mabomba madogo yasiyokdhi mahitaji.

Kutokana na kasoro hizo kubainika Ridhiwani ametoa mwezi mmoja kwa idara ya maji halmashuari ya wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha inafanya marekebisho na ukaguzi wa kina .
Hayo yalijiri juzi,baada ya wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ambao waliambatana na wahandisi kutoka wizara ya maji kumuita mbunge huyo kwa malengo ya makabidhiano ya mradi katika vijiji hivyo.

Akizungumza na wakazi wa vijiji hivyo,Ridhiwani alisema yeye yupo pamoja nao na hawezi kukubali kukubali kupokea mradi ambao una kasoro.
Alitoa siku 30 kupisha marekebisho na ukaguzi na kusema endapo ataridhishwa na marekebisho yatakayofanyika ndipo watakubali kuupokea.

Akielezea kuhusu mradi huo,Ridhiwani alisema ulikuwa wa awali ambapo ulianza mwaka 1997 na kugharimu Mil. 258 kwa fedha za ufadhili kutoka bank ya dunia ambapo 2013 ikiwa ni miaka miaka mitatu sasa ulipaswa ukabidhiwe baada ya kufanyiwa maboresho .

Ridhiwani aliwataka wakandarasi,watalaamu na mhandisi wa idara ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo,Juliana Msagala kuacha masihala kwenye miradi mikubwa inayogharimu kiasi kikubwa cha fedha kutoka serikali na kwa wahisani .

“Hili jambo sio jema linasababisha wananchi wachukie serikali yao hivyo sisi wenye dhama ya uongozi  wajibu wetu ni kuona serikali inaendelea kukaa kwenye sura nzuri na wananchi wakiendelea kujenga imani na serikali yao”

“Mradi huu umeanza 1997 tangu mimi nikiwa namaliza kidato cha nne hadi leo jamani ,hebu rudisha miaka nyuma ni miaka mingapi,wataala jaribuni kufanya kazi kwa maslahi ya jamii na sio kwa maslahi mengine yasiyo na tija”alisema Ridhiwani.

Hata hivyo Ridhiwani alisema oct 2015 mradi huo ulitakiwa ukabidhiwe kwa mara ya kwanza  lakini kwenye ziara ya kamati ya siasa CCM walipita na kuona kasoro mbalimbali na kamati hiyo ilikataa kukabidhiwa .

“Mabomba yalikuwa yanapasuka kwa maana pampu ilikuwa kubwa jawabu ilikuwa kuweka  mabomba yanayofanana na pampu ile na sio kuweka mabomba madogo ya inchi mbili ama tatu ,ni moja kati ya mapungufu,alielezea Ridhiwani.

Alitaja tatizo jingine maji yakijaa wakati wa mvua yakipita kitonga na kufunga barabara ya milo kutokana na mabomba kuchimbwa juu badala ya chini.

Awali Diwani wa kata ya Vigwaza ,Muhsin Baruhan alitoa kasoro mradi huo kutokana na kutotoa maji pamoja na maeneo mengine kuonyesha mipasuko ya mabomba kabla ya kutumiwa na vijiji lengwa.
Alisema wananchi wa vijiji vilivyo ndani ya mradi wanapata tabu hivyo aliwaomba wataalamu kuwa huruma na maisha ya watu ambao wanateseka.
Baruhan alielezea kuwa tayari alishapeleka taarifa za mapungufu ya mradi katika idara husika lakini utekelezaji ndio tatizo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Kidogozelo Ally Mmanga ,kutokana na mradi huo kusuasua kunasababisha wakazi wa kijiji hicho kutumia maji ya madimbwi na mtoni hivyo kuhofia milipuko ya magonjwa na kuliwa na mamba.

Mmanga alisema wanafunzi wa shule hutumia makaratasi kujifutia mara baada ya kujisaidia jambo ambalo linatishia usalama wa afya zao.

Mmoja wa wakazi ,Abdul Saidi mkazi wa Kidogozelo ,alisema bomba lililofungwa ni la inchi mbili ambalo haliwezi kusambaza maji katika mtandao wa vijiji sita hadi kumi kwani kwa kufanya hivyo ni kusababisha maji kutoka kama mkojo.

Katika hatua nyingine mhandisi wa idara ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msagala anasema mradi huo umekamilika kulingana na mkataba licha ya kuhitajika maboresho.

Alisema mradi huo uliingizwa kwenye mpango wa uboreshaji wa mradi katika program ya maji usafi na mazingira vijijini Kidogozelo iliingia katika program ya  vijiji 10 ambapo halmashauri iliingia mkataba na mkandarasi Sajo Engineering Contractor kwa ghamara ya sh mil.258.

Hata hivyo Juliana alisema halmashauri hiyo itamkata mhandisi mshauri mil 18.345 kwa hasara iliyosababishwa na usanifu usio sahihi.

Alisema fedha hizo zitatumika kurudisha mradi wa zamani na kuongeza mtandao wa mabomba katika vijiji vya Kitonga na Kidogozelo.

Mhandisi huyo alikiri kuwepo kwa mapungufu yaliyoonekana na kumuahidi mbunge wa Chalinze Ridhiwani kuwa maagizo aliyoyatoa watayafanyia kazi .

No comments:

Post a Comment