Monday, 8 February 2016

mah5
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Katanga akitoa shukrani baada ya kupokea mfano wa hundi aliyopokea kwa lengo la kusaidia mahakama leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na kulia ni  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
mah6
Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea na kazi yao wakati wa makabidhiano ya fedha hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO
………………………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
 Dar es salaam.
Serikali imeikabidhi Mahakama ya Tanzania kiasi cha Sh.bilioni 12.3 zilizoahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria kwa lengo la kuiwezesha Mahakama kuimarisha utendaji kazi na kutekeleza majukumu yake inapasavyo.
Akikabidhi fedha hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa fedha zilizokabidhiwa kwa Mahakama ni mwitikio wa kutekeleza ahadi ya Rais aliyoitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani Januari 4, 2016.
“Ni matumaini ya Serikali fedha hizo zitatumika vizuri na zitatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa” alisema Dkt. Mpango.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju amemshukuru Mhe. Rais kwa kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa ndani ya siku nne na kuudhihirishia umma kuwa kauli mbiu ya “Hapa Kazi Tu” anaisimamia kwa vitendo.
Naye Mtendaji Mkuu wa Mhakama Hussein Katanga amesema kuwa fedha walizokabidhiwa  zitasaidia ujenzi wa mahakama nchini na zipo ndani ya bajeti ya mwaka 2015/2016 na watazitumia kulingana na malengo yaliyokusudiwa.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu yatoa taarifa ya mfumuko wa bei leo

E1
Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi. Ruth Minja.(Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo)
E2
Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jjijjini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo.
E3
Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa beimapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi. Ruth Minja.

Na Kalonga Kasati
Matumizi ya kaya kwenye biadhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2007.ambapo kwa ujumla wake mfumuko wa Bei umepungu
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizunguza na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei leo jijini Dar es Salaam.

Kwesigabo alisema kuwa kutokana na mwenendo huo kunaashiria kupungua kwa Umasikini Wa kipato kwenye kaya kwa kuelekeza matumizi mengine bidhaa zisizo za vyakula kama usafiri, mawasiliano, makazi, maji na nishati.
“Matokeo yanaonyesha kwamba mizania ya matumizi ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 mwaka 2007” Alisema Kwesigabo.
Aliongeza kuwa makundi mengi mengine yaliyoonyesha kuwa na mizania mikubwa ya Matumizi ya kaya mwaka 2011/12 kuwa ni pamoja na Usafi asilimia 12.5 kutoka asilimia 9.5 Mwaka 2007, Makazi Maji na Nishati asilimia 11.6 kutoka asilimia 9.2 mwaka 2007 na Mavazi na Viatu asilimia 8.3 kutoka asilimia 6.7 mwaka 2007.

Aidha kumekuwa na ongezeko la Zaidi ya mara mbili ya matumizi ya kaya kwenye kundi la Mawasiliano asilimia 5.6 ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya mwaka 2007
Kwa upande wake Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bibi. Ruth Minja amevitaja baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika kupata Fahirisi za Bei zinzoonyesha uhalisia wa matumizi ya kaya binafsi kuwa ni pamoja na mizania katikia bidhaa na huduma muhimu ikiwemo Vyakula, afya, Usafiri ,Maji na Nishati.

Aliongeza kuwa ili kupata matokeo ya mfumuko wa Bei kumekuwa na mtindo wa kufanya marejeo baada ya kila miaka mitano ambapo marejeo ya mwisho yalifanyika mwaka 2007 na kuonyesha matumizi makubwa ya kaya yalikuwa kwenye bidhaa za vyakula zikiwa na asilimia 47.8 ya matumizi yote yakifuatiwa na usafiri asilimia 9.5 huku matumizi madogo zaidi Yalikuwa ni huduma za afya kwa asilimia 0.9.

Takwimu hizi zimekuwa zikitolewa kwa mujibu wa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na Zimekuwa zikisaidia katika kupima na kuboresha sera za kifedha na mipango ya kiuchumi ya kuthibiti mfumuko wa bei, kukadiria pato la Taifa,kuboresha mishahara ya wafanyakazi na Mafao ya wafanyakazi waliostaafu.

TAARIFA KUHUSU MKUTANO WA WADAU WA UWEZESHAJI UTAKAOFANYIKA TAREHE 9/02/2016

logo
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lilianzishwa mwaka 2005 kwa Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Sheria na. 16 ya Mwaka 2004) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Baraza ni chombo cha juu kitaifa cha kuratibu, kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004.
Katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji, Baraza limeshaandaa Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Mwongozo wake unaohusisha sekta zote nchini. Ili kufanikisha utekelezaji wa mkakati huo, Baraza limeandaa Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambao ni muundo rasmi katika kutekeleza Mkakati wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.  Mkutano huu ni sehemu ya Uratibu na utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji ambao unahusisha wadau mbali mbali ambao ni Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa, mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi.
Mkutano huu wa Wadau wa Uwezeshaji utafunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Majaliwa Kassim Majaliwa (MB), tarehe 9/02/2016 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.
MAJUKUMU YA BARAZA
  1. Kuandaa Mpango Mkakati wa Kisekta na kuhamasisha matumizi ya rasilimali kwa shughuli za uwezeshaji wananchi;
  2. Kuhamasisha na kuhimiza uwekaji wa akiba, uwekezaji na ushirikishwaji makini wa wananchi kwenye shughuli za kiuchumi;


WAZIRI UMMY MWALIMU AWASHUKIA WANAOTOA HUDUMA ZA AFYA KINYUME CHA SHERIA

NUMMY
Dar es salaam

Na Kalonga Kasati

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyataka Mabaraza na Bodi za kitaalamu za masuala ya afya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wataalam na vituo vinavyotoa huduma za afya kinyume cha Sheria.
Waziri Ummy ametoa agizo hilo alipokuwa akizindua Baraza la Optimetria, Baraza la wataalamu wa Radiolojia pamoja na Bodi ya Maabara binafsi leo jijini Dar es salaam.
Alisema kisheria Mabaraza na Bodi za Kitataalam ndivyo vyombo vinavyofuatilia ubora wa huduma za Afya pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuwaepuka watoa huduma batili wasiokuwa na utaalam na ujuzi wala kukidhi vigezo vya utoaji huduma vilivyowekwa kisheria.
“Siku hizi kumekuwa na matumizi makubwa ya vyeti vya kugushi vikiwemo vya vituo vya kutolea huduma na wataalamu, watu wasio na taaluma wanatoa huduma kinyume na sheria hivyo Mabaraza na Bodi  mna mamlaka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu,” Alisema Waziri Ummy.
Aidha, alisema kuwa Serikali haitasita kuyachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuvunja Bodi au Mabaraza yatakayoshindwa kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika sheria iliyohusika kuyaanzisha.
Aliyataka mabaraza hayo kuhakikisha kuwa yanatoa Elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na ufahamu kuhusu huduma bora za afya zitolewazo na wataalamu  husika.
“Wananchi wakielimishwa wataepuka  watoa huduma batili wasiokuwa na utaalamu na ujuzi hivyo mabaraza na Bodi vinapaswa kuhakikisha mambo haya hayatokei  kwani vinauwezo mkubwa wa kufuatilia masuala haya kwa mujibu wa Sheria”alifafanua Waziri Ummy.
Akizungumza kuhusu utendaji kazi wa wataalamu hao Waziri Ummy amewataka wataalamu hao kujiendeleza kielimu kwani utaalamu bila kuwa na ujuzi ni butu hivyo suala la elimu lipewe kipaumbele.
Mbali na hayo Waziri ameitaka Mabaraza na Bodi kuhakikisha wataalamu wote, vifaa na vitendanishi vinasajiliwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.

No comments:

Post a Comment