Friday 26 February 2016

Waziri Kitwanga Akutana na Vionozi wa nida awataka kuongeza kasi Uandaji wa Vitambulisho vya Taifa

KTG1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza upande wa kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KTG2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wizarani hapo, Haji Janabi. Wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba, anayefuata ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KTG3
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modest Kipilimba akijitambulisha kabla ya kuanza kikao cha Watendaji Wakuu wa NIDA pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kikao hicho kilichoitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na anayefuata ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KTG4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza jambo katika kikao kazi alichokitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya NIDA na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa tano kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modest Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI

JAN1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba (kushoto) akiongea na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Al-Najem, Balozi huyo alimtembelea Mh. Makamba Ofisini kwake leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana masuala ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira.
JAN2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba (kushoto) akiongea na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Al-Najem, Balozi huyo alimtembelea Mh. Makamba Ofisini kwake leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana masuala ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makumu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Barthlomew Jungu.

Badilisheni Sera zenu Muandike Habari chanya kwa watu wenye Ulemavu: Dkt Possi

PO1
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt  Abdallah Possi akizungumza na Wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari leo ofisini kwake Jijini Dare s salaam.
PO2
Mhadhiri toka Chuo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Shule ya Uandishi wa Habari Dkt Harub Riyoba (katikati) akimsikiliza Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt  Abdallah Possi alipokutana na Wamiliki wa Vyombo vya habri kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji toka Azam Media Yahya Mohamed na kushoto ni Meneja wa Uendeshaji toka Sahara Media Steve Diallo.


Na Kalonga Kasati
 
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt  Abdallah Possi ameviagiza vyombo vya habari nchini kuwa na sera katika vyombo vyao inayojumuisha uandishi wa habari chanya kwa watu wenye ulemavu.
 
Akitoa agizo hilo mbele ya wamiliki wa vyombo vya habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Waziri Possi amesema habari nyingi zinazohusu watu wenye ulemavu ni za kuwanyanyapaa na kuonesha kuwa hawana uwezo wa kufanya mambo chanya.
 
“Wekeni kipengele katika sera zenu kitakachosaidia kuwaelimisha watu kuwa watu wenye ulemavu ni sehemu ya jumuiya katika maisha ya kila siku ya wanadamu,” amesema.
Kwa mujibu wa Waziri Possi, vyombo vya habari vikiwa na sera iliyowazi na kuitekeleza, watu watabadilika na kupata taarifa nzuri za watu wenye ulemavu.
 
Dkt. Possi ameeleza kuwa taarifa za watu wenye ulemavu hazitakiwi kuwa na lugha zenye chembechembe za kunyanyapaa.
 
Amesema kuwa kila kituo cha televisheni kinatakiwa kuwa na wataalamu wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama.
 
Amesema, “Serikali kwa kutumia Sheria ya Watu wenye ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 inaandaa tangazo kuvikumbusha vyombo vya habari kuwa kuwa na wataalam wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu.” 
 
Aidha Naibu Waziri amewaagiza wamiliki wa vyombo vya habari kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu kwani Sheria inaagiza lazima chombo chochote chenye wafanyakazi zaidi ya 20, angalau mfanyakazi mmoja awe mtu mwenye ulemavu.
 
Kwa upande wao wamiliki wameiomba serikali kutotoza kodi tangazo lolote linalohusu habari chanya za watu wenye ulemavu.
 
Hata hivyo wamiliki hao wamemweleza Naibu Waziri kuwa ubadilishaji wa Sera pamoja na kuwa na wataalam wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa watu wenye ulemavu ni jambo zuri, lakini wanahitaji kupewa muda wa maandalizi.

No comments:

Post a Comment