Monday 22 February 2016

Gavana amezindua Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa Elimu na Ulinzi kwa Mtumiaji wa Huduma za Fedha

bot1
Meza kuu ikifuatilia kwa makini yanayojiri katika kikao cha uzinduzi wa Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF).
bot2
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
bot3
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania akieleza jambo wakati wa uzinduzi Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF).
bot4
Bi. Susan Rutledge, Mtafiti na Mshauri wa masuala ya fedha, akieleza umuhimu wa elimu ya masuala ya fedha kuelekezwa kwa wananchi.
Na Kalonga Kasati
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Kifedha Tanzania (FSDT), imezindua Mwongozo wa taifa wenye lengo la kuongeza uelewa kuhusu elimu ya mambo ya fedha kwa wananchi.
Uelimishwaji wa wananchi kuhusu mambo ya fedha utatekelezwa kupitia “Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF). 

Gavana Prof. Beno Ndulu ameuzindua rasmi mwongozo huu ambao utajikita katika kutatua changamoto zilizobainishwa katika utafiti uliopima uelewa wa mambo ya fedha kwa watu wazima nchini Tanzania. Utafiti huu unaitwa “Uwezo wa Kifedha Tanzania” wa mwaka 2014. 

Utafiti huo umebainisha kuwa watanzania wengi hawana elimu na ujuzi mahususi wa  masuala ya mambo ya fedha kwa ujumla, hivyo kuwanyima fursa ya kutumia huduma za kifedha kwa faida yao.
Katika utafiti huo imeonyeshwa kuwa upatikanaji wa huduma za fedha umekuwa na changamoto katika maeneo mengi huku zile zitolewazo kwa njia ya mitandao bado hazikidhi matarajio ingawa zinawafikia  wateja wengi kwa sasa. 

Sambamba na hilo kumekuwa na uhaba wa nyenzo na miundombinu ya kuhifadhi na kufikisha taarifa za fedha kwa watumiaji wa huduma hizo  kwa kuzingatia namna sahihi ya kutoa taarifa, kuwaelimisha na kuwalinda.

Kutokana na utafiti wa “Uwezo wa Kifedha Tanzania” wa mwaka 2014 wananchi kutoka makundi mbalimbali katika jamii hawana ujuzi wa hesabu za kawaida  ambao ndiyo msingi mkuu katika nadharia ya masuala yahusuyo mambo ya fedha.  

Elimu msingi katika masuala ya fedha umekuwa kikwazo kwa waliowengi  hasa katika uandaaji wa bajeti, kutunza kumbukumbu ya matumizi, kupanga fedha kwa matumizi yasiyotegemewa ama ya ziada na muhimu zaidi kutunza kiasi kwa ajili ya matumizi ya uzeeni (baada ya kustaafu).
Inaonekana kuwa upatikanaji wa taarifa za masuala ya fedha hutegemea zaidi vyombo vya habari kama redio, televisheni na magazeti lakini vyombo hivi kwa sehemu kubwa,  hufikisha zaidi taarifa Za biashara na masoko kuliko ambavyo vinaelimisha jamii kuhusu matumizi na Upangaji wa mapato yao.

 “Haya ndiyo masuala mahususi ambayo  mwongozo huu wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha unalenga kushughulika nayo,” alisema Prof Ndulu.

Pamoja na kuwepo ongezeko la upatikanaji wa huduma za kifedha, mpaka asilimia 58  mwaka 2013 kutoka kiwango cha asilimia 17 mwaka 2009, miongoni mwa watu wazima nchini, bado Mwongozo huu ni muhimu ili kuleta mfumo imara wa sekta ya fedha na Zaidi sana ili kuleta ustawi wa maisha ya watanzania kwa ujumla.

Prof. Ndulu anasema kutatua changamoto za kielimu kwa ujumla na hususan elimu ya huduma za Fedha italiwezesha taifa kuwa katika mwelekeo mzuri wa kukabiliana na umasikini na kufikia malengo ya kukuza uchumi.

 “Tunapaswa kujiuliza: ni kwa namna gani wananchi hasa wale masikini na wasiokuwa na elimu za kifedha  za wanapambana kuendeleza biashara zao katika mazingira ya soko huria na lenye ushindani kila uchwao” alisisitiza Prof. Ndulu.

Hivyo, mwongozo huu utahakikisha watanzania wapata elimu sahihi na ya uhakika ya huduma za kifedha pamoja na njia anazoweza nazo kujilinda katika ushindani huu.
Vilevile mwongozo huu umeundwa ili kutatua changamoto za kifedha zinazohusiana na maamuzi Miongoni mwa watumiaji wa huduma hizi na kuwa jumuishi na wenye tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mwongozo wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha umeandaliwa kwa kujumisha washikadau kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
Unabainisha changamoto zinazohusuana na uwezo wa kifedha ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa uwepo wa elimu ya fedha. Pia, unatoa taratibu wakufanikisha utekelezaji wa elimu ya fedha, na mwongozo wa kitaifa wa kuratibu elimu ya fedha nchini.
Lengo la mwongozo wa elimu ya huduma za fedha ni kuwa na wananchi na kaya zenye uwezo kifedha nchini.

Kikwete Amezindua Ofisi Ya CCM Wilaya Ya  Kibaha Mjini Leo

kib1
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizindua Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha mjini mkoani Pwani leo. Ofisi hiyo imejengwa na familia ya Mbunge wa Kibaha mjini Slyvester Koka (kulia). .

Kombe  La Shirikisho Kuendelea  Wiki Hii

Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuendelea wiki hii mzunguko wa nne katika hatua ya 16 bora, kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.

Jumatano Februari 24, 2016 kutakua na mchezo mmoja tu, ambapo timu ya Young Africans watawakaribisha maafande wa JKT Mlale kutoka mkoani Ruvuma katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezwa majira ya saa 10:30 jioni.

Michezo miwili itachezwa siku ya Ijumaa ambapo, Ndanda FC watakua wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Nagwanda Sijaon mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Jumamosi Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, wakati jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo.

Mzunguko huo wa nne utakamilika siku ya Jumapili ambapo, Simba SC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

NB: Rais wa TFF, Jamal Malinzi kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi, ataongea na waandishi wa habari katika Ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.

DK Shein  Amezungumza  Na  UVCCM Mkoa  Wa  Mjini

ccm1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Mjini kichama leo katika ukumbi wa CCM Amani Mjini Unguja na kuwataka Vijana kulinda Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar,ikiwa ni katika hatua za uimarishaji wa Chama cha Mapinduzi,[Picha na Ikulu.]

Makamu  Wa  Rais  Akutana Na  Ujumbe Wa  Watu Wa China Na  Mwenyekiti  Wa  Shell Deep

ras1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan  akizungumza na Ujumbe wa kampuni ya Gezhouba kutoka China kuhusu masuala ya uwekezaji. Kushoto ni kiongozi wa msafara huo Mhandisi Hu pend.

No comments:

Post a Comment