Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla
akisisitiza suala la Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu
kusini- Mbeya kununua mashine ya CT-scan ndani ya siku 60, huku akiahidi
kuwachukulia hatua kali ya kuwawajibisha watendaji watakaozembea katika
hilo.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipita katika moja ya maeneo ya
hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya sambamba na wenyeji wake…
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla
amefanya ziara, Februari 12, 2016 katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya
Nyanda za juu kusini- Mbeya, na kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo
upatikanaji wa mashine CT-Scan ndani ya siku 60 huku akibainisha kuwa
endapo watazembea basi watawachukulia hatua kali na kuwajibishwa
watendaji na uongozi wa Hospitali hiyo.
Dk.
Kigwangalla alifika hospitalini hapo majira ya saa tisa alasiri na
kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji
kazi ambapo ndipo alipobaini ukosefu wa mashine hiyo ya CT-Scan pamoja
na vifaa vingine muhimu ambavyo alibainisha kuwa hata uongozi wa
Hospitali hiyo walikuwa na uwezo wa kuvinunua bila kutegemea Serikali.
Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla
alitembelea ni pamoja na kitengo cha kutolea huduma kwa wagonjwa (OPD),
Kitengo cha upasuaji, wodi ya upasuaji, duka la dawa la hospitali hiyo,
wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, watoto na kitengo cha Maabara ambapo
kisha alipata kuongea na wafanyakazi pamoja na uongozi mzima wa
Hospitali.
Dk.Kigwangalla
alitoa wasaha mwingi kusikiliza kero za wafanyakazi hao kuongea lile
linalowakabili bila kuogopa ili aweze kujua matatizo na changamoto
zinazowakabili.
“Hospitali
kubwa kama hii hapa Mbeya na wataalam wote mlionao mnashindwa kufanya
biashara!, Mnategemea tu Serikali? lini mtakuwa na CT-scan kwa upande
wenu? wakati mnaingiza Milioni 500 kwa mwezi?” alihoji Dk. Kigwangalla.
Dk.Kigwangalla
aliwaambia uongozi wa hospitali hiyo ina fursa na uwezo wa kufanya
jambo kubwa kwani pia ina uwezo hata wa kukopa fedha kutoka mashirika ya
bima ya afya.
Aidha, Dk Kigwangalla amewataka
uongozi wa Hospitali hiyo kuwa wabunifu katika uendeshaji wao ikiwemo
kutengeneza jengo la kisasa la matibabu ya kulipia, kujenga nyumba za
wafanyakazi ambapo amewapa mikakati hiyo imeanza na pindi atakaporejea tena hospitali hiyo.
MuonekanoWaKituo Kipya Cha Kusuma Maji Ruvu Darajani Kikiwa Kimekamilika
Pampu moja ya kituo hicho inauwezo
wa kusukuma maji lita milion 60 kwa siku kuna jumla ya pampu mpya tatu
na pampu mbili zitakuwa zinafanya kazi kwa wakati mmoja.
No comments:
Post a Comment