Tuesday 23 February 2016

Waziri Wa Uchukuzi na Ujenzi Makame Mbarawa ametoa Mwezi Mmoja kwa Makandarasi nchini

mbr1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kuhusu ukusanyaji madeni ambayo Wakala wa Majengo nchini (TBA) inadai wapangaji wake.
mbr3
Muonekano wa barabara ya Sakina-Tengeru Km 14.1 inayojengwa kwa njia nne kwa kiwango cha lami ili kupunguza msongamano wa magari kuingia na kutoka katikati ya jiji la Arusha.
mbr2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi M/S Hanil Jiangsu J/V anayejenga barabara ya Sakina-Tengeru Km 14.1 na barabara ya mchepuo wa kusini Arusha bypass Km 42.4 jijini Arusha.
mbr5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akikagua ripoti ya biashara inayofanywa na Kampuni ya Simu nchini (TTCL), jijini Arusha. Wa tatu kulia ni Meneja Kanda ya Kaskazini TTCL Bw. Peter Lusama.
mbr6
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiimba wimbo wa mshikamano daima na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS kabla ya kufungua rasmi mkutano wa sita wa Baraza hilo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Fadhili Nkurlu.
mbr7
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza kufanya kazi kwa malengo yanayopimika katika kikao chake na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake, jijini Arusha.
mbr8
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisikiliza maelezo ya namna ya kuhamisha miundombinu ya maji pembeni ya Barabara ya Sakina-Tengeru
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa Makandarasi wote nchini kuhakikisha wanasaini mikataba ya ajira na wafanyakazi katika miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea nchini kote.

Akizungumza jijini Arusha mara baada ya kufanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa Km 14.1 na barabara ya mchepuo ya kusini (Arusha bypass) yenye urefu wa Km 42.4, Prof. Mbarawa amesema mkandarasi atakayeshindwa kutoa mikataba kwa mujibu wa sheria za Tanzania, atanyang’anywa kazi ya ujenzi kwa kuvunja sheria.

“Barabara zinajengwa kwa kodi za wananchi hivyo wajenzi wa barabara nao ni lazima wafuate sheria za nchi ili kuhakikisha Serikali inapata kodi stahili na wafanyakazi wazawa nao wanapata haki stahili kwa mujibu wa ajira zao”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Amezitaka taasisi za TRA, NSSF na nyingine zinazosimamia ajira za wafanyakazi kufuatilia miradi ya ujenzi ili kuona fursa za mapato ambazo serikali inaweza kupata na kusajili wafanyakazi katika hifadhi ya mifuko ya jamii.

Waziri Prof. Mbarawa amewataka mameneja wa tanroads na maafisa kazi kukagua mikataba ya Ajira za ujenzi katika maeneo yao ili kuona haki inatendeka kwa makandarasi na kwa Wafanyakazi ili ujenzi wa barabara ukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amefungua mkutano wa Sita wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na kuwataka kuweka mikakati itakayowezesha kulinda hifadhi ya barabara, kudhibiti magari yanayozidisha uzito na kusimamia kasi katika miradi ya ujenzi wa barabara.

“Mmekua mkifanya kazi nzuri, endeleeni kufanya kazi kwa uadilifu, uwazi, weledi na kujiwekea Malengo ya kujipima mwaka hadi mwaka ili muendelee kuwa tassisi ambayo watu watakuja kujifunza kwenu”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa TANROADS imejipanga kuhakikisha miradi ipatayo 90 ya ujenzi wa barabara inayoendelea nchini kote inakamilika katika ubora unaotakiwa na unao uwiana na thamani ya fedha.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoa Wa Arusha, Bw. Victor Baltazar kukusanya madeni yote kwa haraka ili kukamilisha miradi ya Ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na za biashara inayosimamiwa na Wakala huo mjini Arusha kukamilika kwa wakati.
Prof. Mbarawa ambaye yuko katika ziara ya mikoa ya kanda ya kaskazini amezitaka taasisi zilizo chini wa wizara hiyo kuhakikisha zinafanya kazi kibiashara ili kuboresha mapato ya Serikali na hivyo kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC NA UNDP ZAFANYA MIKUTANO YA MAJADILIANO KUBORESHA UTOAJI ELIMU YA MPIGA KURA

KALIMANI
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima alipozindua kituo Cham mawasiliano ambapo Jumla ya Simu 1,381 zilipokelewa katika kituo cha Mawasiliano cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi – Nec Call Center, kilichoanzishwa mahususi kwa lengo la kuwasaidia wapiga kura pamoja na wadau mbalimbali wa uchaguzi ili kupata elimu ya mpiga kura.

Na Mwandishi Wetu

Hivi karibuni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Mradi wa ukuzaji wa Demokrasia nchini (DEP) chini ya shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) iliandaa mikutano ya tathmini ya utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura  wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana ili kujadiliana juu ya kuboresha utoaji wa Elimu hiyo katika Chaguzi na kuboresha ushirikiano kati ya Tume na Wadau mbalimbali wa Uchaguzi.

Mikutano hiyo pia ililenga kuainisha maeneo ambayo wadau wanataka yafanyiwe marekebisho ili  kuboresha utendaji kazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kukuza Demokrasia nchini na kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa Chaguzi.
Mikutano hiyo ilifanyika kwa Kanda kwa kuwashirikisha Mwenyekiti wa Tume na Makamishna, Mkurugenzi wa Uchaguzi Wakuu wa Idara pamoja na Maafisa Kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi na Mikoa iliyoalikwa kwenye Mkutano huo.

Mikutano hii ilifanyika kuanzia Februari 2 hadi 11, mwaka huu katika miji ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Lindi, Mtwara, Mbeya, Rukwa na Katavi. Miji mingine ni pamoja na Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Unguja, Pemba, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Mara, Simiyu,  Ruvuma, Njombe na Iringa.

Aidha, Mikutano hiyo ilishirikisha wadau mbalimbali wa Uchaguzi wakiwemo wawakilishi wa Asasi za Kiraia wa makundi mbalimbali ya jamii kama vile Wanawake, Vijana, Watu wenye Ulemavu, na Wazee. Wengine ni Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa (Regional Election Coordinators), Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo ambao pia ni Wakurugenzi wa halmashauri (Rertuning Officers), Maafisa Uchaguzi na Maafisa Habari kutoka kila Halmashauri ulipofanyika mkutano wa wadau.

Kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imepewa jukumu la kutoa Elimu ya Mpiga Kura na kusimamia Asasi, Makundi au watu wanaotoa Elimu hiyo. 
Kwa kuzingatia umuhimu wa jukumu hilo, Tume ilishirikisha Asasi za Kiraia 447 katika kuhamasisha wananchi na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kushiriki na kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na pia kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Asasi za Kiraia ni wadau wakubwa katika mchakato wa Uchaguzi kwa kuzingatia ukweli kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi peke yake haiwezi kuwafikia Watanzania wote kutokana na kutokuwa na rasilimali watu ya kutosha katika kuwafikishia Elimu ya Mpiga Kura pamoja na utaalamu mbalimbali wa utoaji wa Elimu hasa jinsi ya kuwafikia watu wenye mahitaji maalumu kama walemavu, wanawake, vijana pamoja na wale walioko pembezoni na maeneo yasiyofikika kwa urahisi kwa sababu mbalimbali zikiwemo za miundombinu

No comments:

Post a Comment