Tuesday 16 February 2016

Waziri wa Elimu amfuta kazi Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo

Waziri Wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako.
Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa kazi Wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo  George Nyatenga. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo  George Nyatenga.
Pia amewasimamisha kazi Wakurugezi watatu wa Bodi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo.
 
Prof Ndalichako  Amemwagiza Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali ahakiki Maelezo na Nyaraka Zilizowasiliwa na Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya Ukaguzi Maalum kwa kipindi cha kuanzia Mwaka 2013 hadi sasa.

No comments:

Post a Comment