Thursday 25 February 2016

Zuma awasili Burundi kwa mazungumzo


 Zuma
Rais Zuma na Rais Nkurunziza wakikagua gwaride uwanja wa ndege Bujumbura
Viongozi watano wa nchi za Afrika, wakiongozwa na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, wamewasili Burundi kujaribu kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini humo.

Ujumbe huo Unaoongozwa unajumuisha Marais wa Gabon Ali Bongo Ondimba, Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, Senegal Macky Sall na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.

Ziara yao inajiri siku chache tu baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuzuru Taifa hilo na kumhimiza Rais Pierre Nkurunziza akubali Mazungumzo.

Umoja wa Afrika umekuwa ukiishinikiza Burundi kukubali kushiriki mazungumzo na viongozi wa upinzani ili kumaliza machafuko yaliyoanza Aprili mwaka jana.

Machafuko hayo yalitokana na hatua ya Rais Pierre Nkurunziza ya kutangaza kwamba angewania urais kwa Muhula wa tatu. Aliwania baadaye na kushinda.
Rais Nkurunziza na Rais Zuma 
 
 
 
Zuma
 
Hali ilizidishwa na jaribio la mapinduzi ya serikali mwezi Mei ambalo lilifeli.
Watu zaidi ya 400 wamefariki na maelfu wengine kutoroka makwao tangu Aprili mwaka jana.
Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Prime Ndikumagenge anasema uwanja mkuu wa ndege wan chi hiyo leo umekuwa na shughuli nyingi.

Viongozi hao watano wamewasili wakitumia ndege zao za kibinafsi.
 
Rais Nkurunziza na Rais Ali Bongo 
 
 
Nkurunziza
 
 
Bw Zuma, kabla ya kuwasili, alituma ndege mbili za kijeshi za kubeba mizigo ambazo zilikuwa na magari ya kijeshi ya kutumiwa na maafisa wa kulinda usalama wake.

Viongozi hao, waliolakiwa na mwenyeji wao Rais Nkurunziza, hawakuhutubu baada ya kuwasili.
Viongozi hao wanatarajiwa kuishinikiza serikali ya Rais Nkurunziza kukubali mazungumzo yatakayoshirikisha Pande zote kwenye mzozo huo.

Waziri wa Mashauri ya kigeni wa Burundi Alain Aime Nyamitwe amesema serikali hiyo inakubali Mazungumzo Japo kwa masharti.

No comments:

Post a Comment