Friday 19 February 2016

DDCA yachimba visima 52 na mabwawa 3 siku 100 za rais Dkt. Magufuli

KD1
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa Bw. Egwaga Nungu akiongea na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) na kuwaeleza kuhusu Mafanikio waliyoyapata Katika Siku 100 za uongozi wa Rais John Pombe Magufuli ikiwamo kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu mbalimbali nchini, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Saalam, Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari-MAELEZO Bi. Lilian Lundo

NA Kalonga Kasati
Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA) wamefanikiwa kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu mbalimbali nchini Katika Siku 100 za uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Hayo yamesemwa  na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa Bw. Egwaga Nungu wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

 “Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA) katika kipindi cha kuanzia Novemba hadi februari tumeweza kufanikiwa kuchimba visima 52 zitakavyowezesha kupataikana kwa maji safi kwa watanzania katika maeneo mbalimbali na pia wakala umefanikiwa kuchimba mabwawa 3” Alisema Bw. Egwaga.

Akiongelea Matarajio na mipango ya wakala Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Bw. Egwaga amesema kuwa wakala unatarajia kuchimba visima 400, kupima wingi wa maji katika maeneo 420, kusafisha visima 500, pumping installation visima 400 na kukarabati visima 100.

Katika kipindi cha miaka kumi wakala wamefanikiwa kuongeza cha maji kwa jamii kwa wastani wa 53,823m3 za maji kwa siku na kufikia wastani wa asilimia 86 na kuwawezesha wananchi kupata vyanzo vya maji safi na salama kupitia uchimbaji wa visima.

YANGA v SIMBA KESHO TAIFA

Tiketi za mchezo wa watani wa jadi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC Jumamosi, Februari 20, 2016 zimeanza kuuzwa leo Ijumaa saa 2 asubuhi leo asubuhi katika vituo 10 mbalimbali vilivyopo jijini Dar es salaam.

Vituo vinavyotumika kuuza tiketi za mchezo huo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni Oilcom, Ubungo Oilcom, Uwanja wa Taifa Temeke, Mavuno House – Posta, Dar Live Mbagala, Breakpoint – Kinondoni, Kidongo Chekundu – Mnazi Mmmoja, Mwenge na Kivukoni Ferry.
Kiingilio cha juu cha mchezo huo ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.

Milango ya Uwanja wa Taifa itafunguliwa kuanzia saa 5 kamili asubuhi, huku barabara ya Chang,ombe ikifungwa kuanzia asubuhi, na magari maalumu yenye stika maalumu ndiyo yatakayoruhushiwa kuingia eneo la uwanja wa Taifa kwa kupitia barabara ya Mandela na uwanja wa Uhuru.

Upande wa ulinzi, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama watakuwepo kuhakikisha usalama wa wapenzi wa mpira watakaokuja kushuhudi mchezo huo, vitu kama silaha, vilevi, mabegi na vitu vyenye ncha havitaruhusiwa kuingia ndani ya uwanja.

Shirikisho linawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini kununua tiketi katika magari ya kuuzia tiketi katika vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizo halali kwa mchezo huo.

Mchezo huo utachezeshwa na mwaamuzi Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na mwamuzi Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha) wote wakiwa wakiwa waaamuzi wenye beji za FIFA, mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) na Kamisaa wa mchezo huo atakua Khalid Bitebo (Mwanza).

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UJUMBE WA WABUNGE MAREKANI

UJ01Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Marekani (Congress) waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Febuari, 2016.
UJ1Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakizungumza na Ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Sweden waliotembelea Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam.
UJ02Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Marekani (Congress) waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
UJ2Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wkiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Sweden waliotembelea Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment