Friday 19 February 2016

Ukataji wa Tikect kwa ajili ya kuangalia mechi Uwanja wa Taifa kwa njia ya Elekroniki waiva.

tik1
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura ((wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TFF, BMT na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mara baada ya kumaliza  wa kikao  kilichofanyika ofisinii kwake leo jijini Dar es Salaam.Kikao hicho kimefanyika ili ya kujadili suala la matumizi ya mashine za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi wakati wa mechi kwenye uwanja wa Taifa.

tik2
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza katika kikao baina yake na uongozi kutoka TFF na BMT ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujadili suala la matumizi ya mashine za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi wakati wa mechi kwenye Uwanja wa Taifa.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Dioniz Malinzi na kulia ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
tik3
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akifuatilia maelezo kutoka kwa Muhasibu Mkuu wa Wizara  hiyo Bibi. Rose Janeth Bandisa (kulia) wakati wa kikao  baina yake na uongozi kutoka TFF na BMT ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kikao hicho kimefanyika ili ya kujadili suala la matumizi ya mashine za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi wakati wa mechi kwenye Uwanja wa Taifa.Katikati ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
tik4
Katibu Mkuu wa TFF Celestine Mwesiga (kushoto) na Muhasibu Mwandamizi wa TFF Bw. Daniel Msangi wakifuatilia kwa makini wakati wa kikao baina yao na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
tik5
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) akizungumza katika kikao baina ya  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (katikati) na uongozi kutoka TFF na BMT leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
tik6
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja akizungumza  wakati wa  kikao baina ya  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (katikati) na uongozi kutoka TFF na BMT leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

MAGUGU MAJI YATISHIA HUDUMA ZA USAFIRI ENEO LA KAMANGA FERRY JIJINI MWANZA.

Vita ya Kupambaza na Uwepo wa Magugu Maji katika Maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria, bado haijazaa matunda Chanya. 
 
Suala la kupambana na magugu maji katika ziwa hilo bado ni changamoto, licha ya kuwepo kwa Miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Uhifadhi wa Mazingira ya Bonde la Ziwa Victoria (LIVEMPT I & II) iliyolenga kuokoa uwepo wa Ziwa Victoria ambayo pia ililenga kupambana na magugu maji.
 
Mara kadhaa huduma za usafirishaji katika Kivuko cha Busisi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, zimekuwa zikitatizwa na uwepo wa Magugu maji ambayo hutanda katika eneo la ferry la kivuko.
 
Usumbufu kama huo unahofiwa huenda ukajitokeza katika eneo la Kamanga Ferry Jijini Mwanza, baada ya Magugu Maji kugonga hodi na kuanza kutanda katika eneo hilo.
 
Kumbuka Magugu maji yanaweza kutambaa kutoka eneo moja hadi jingine kulingana na upepo unavyovuma na yanaweza kuleta athari ya usafirishaji majini ikiwa chombo cha usafiri (Meli/Ferry) kitanasa katika Magugu maji.
 
Suala kubwa ni kuhakikisha mapambazo zaidi dhidi ya magugu maji yanaendelea ikiwemo kuvitumia vikundi vya Kusimamia Rasilimali za  Uvuvi katika Ziwa Victoria (Beach Management Unit-BMU) ambavyo mara moja moja pale vinapowezeshwa, vimekuwa vikifanya shughuli ya kutoa magugu maji Ziwani.
 
Hata hivyo jitihada za vikundi hivyo zimekuwa zikikwama kuleta suluhisho maana magugu maji yanapotolewa majini, ni vyema yakachomwa moto jambo ambalo huwa ni nadra kufanyika na matokeo yake magugu maji hayo hurudi ziwani kwa njia moja ama nyingine, ikiwemo kwa njia ya shughuli za kilimo katika maeneo ya kandokando mwa ziwa Victoria.
Shughuli za Kupambana na Magugu Maji zikifanyika eneo la Nera Jijini Mwanza mwishoni mwa Mwaka jana

Wakaazi wa kisiwa cha Mtambwe Mkuu Wilaya ya Wete waomba taasisi za kupambana na uharibifu wa mazingira kuelekeza nguvu kisiwani humo

images (6)Na Tabu Mullah
WAKAAZI wa kisiwa cha Mtambwe Mkuu Wilaya ya Wete wameziomba taasisi zinazoh
usika na suala la utunzani wa  mazingira kuelekeza nguvu katika kisiwa hicho ambacho kiko hatarini kutoweka .
 
Wamesema kwamba kisiwa hicho kimekuwa kikiliwa na maji ya bahari siku ha siku , na kusababisha eneo la kisiwa hicho kupungua kwa kasi .
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi  wamesema iwapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa na Serikali pamoja na taasisi husika , historia ya kisiwa hicho itapotea .
 
“Kisiwa hichi kinahistoria kubwa , lakini inaweza ikapotea kutokana na bahari kuendelea kuvamia ardhi ya kilimo na makaazi , tunaomba nguvu katika kufanikisha hili ”alisema Alawi .
Sheha wa Shehia ya Mtambwe Kaskazini Bakar Khamis Suleiman ameiomba Serikali pamoja na taasisi binafsi kuweka  mkazo wa kupanda miti ya kudumu kwenye eneo la kisiwa hicho .
 
Sheha Bakar amesema wakaazi wa kisiwa hicho wamekuwa wakipanda miti , lakini kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha miti imeshindwa kutatua tatizo hilo .
 
“Kipo kikundi cha upandaji wa  miti katika Kisiwa hichi , lakini mafanikio hayapafikiwa kutokana na wanakikundi hao kukosa taaluma na miti wanayopanda imeshindwa kutatua tatizo ”alifahamisha .
 
Inakisiwa kwamba eneo la zaidi ya mita ishirini na nchi kavu zimekuwa himaya ya bahari katika Kisiwa hicho , ambapo miti aina ya miembe na minazi nayo ikiwa imeng’olewa na mawimbi ya bahari .
 
Kwa upande Mwenyekiti wa Jumuiya ya wandishi wa Habari  wa Mazingira Pemba Azizi Smail Alawi ameahidi kuwa Jumuiya yake imejipanga kutoa elimu ya upandaji wa miti hasa maeneo ya visiwa vidogo vidogo .
 
Amesema kwamba shehia nyingi ambazo ziko kando kando ya bahari , zimevamiliwa na maji na kuzitaja kuwa ni Msuka ,Mjini Kiuyu pamoja na  Kisiwa Panza

No comments:

Post a Comment