Jeshi La Polisi Limejipanga Kuimarisha UlinziWakati Wa Upigaji Kura Kwenye Uchaguzi Wa Marudi Zanzibar
Kamishna wa Jeshi la Polisi
Zanzibar Hamdan Omar Makame amesema kwamba Jeshi hilo limejipanga
kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya Unguja na Pemba wakati wa
upigaji kura kwenye uchaguzi wa marudio .
Akizungumza na Gazeti hili
Kisiwani Pemba Kamishna Hamdan amewatoa hofu wananchi kuwa hakuna Mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura ambaye hataweza kwenda kupiga kura Tarehe 20 machi mwaka huu wakati wa uchaguzi wa marudio kutokana na
sababu za vitisho .
Amesema kwamba tayari Jeshi la
Polisi limeanza kutengeneza mazingira ambayo yatawaweza wananchi kila
mmoja kuwa huru na kuhakikisha kuwa usalama wa nchi utaendelea
kudumishwa .
Katika Mazungumzo na gazaeti hili katika Makao Makuu wa Jeshi hilo Mkoa wa
Kaskazini Pemba , Kamishna Hamdan amefahamisha hakuna mwananchi ambaye
hatapiga kura kutokana na vitisho , labda aache kwa sababu zake mwenyewe
.
“Hakuna
mwananchi ambaye atapata fursa ya kupiga kura kwa sababu za vitisho ,
labda yeye Asiende kwa sababu anazozijua yeye , lakini sio suala la
vitisho ulinzi utaimarishwa maeneo yote ya Unguja na Pemba ”alisisitiza
Hamdan .
Aidha
Kamishna Hamdan amesema pamoja na kazi ya ulinzi wa wananchi na mali
zao kuwa Ni Polisi , lakini iko haja kwa wananchi nao kuwapa
ushirikiano askari pindi wanapobaini kuwa viasharia vya vitisho au
uvunjifu wa amani .
Ameeleza
kwamba ni kazi ya Jeshi la Polisi kuona wanannchi wanaishi kwa amani
katika nchi Yao na wanafanya mambo kwa mujibu wa sheria , na kuongeza
tayari changamoto Zinazojitokeza ikiwemo vitisho wanazifahamu na
wanazifanyia kazi ili zisilete Athari wakati wa zoezi la uchaguzi .
“Niwahakikishie
wananchi kwamba changamoto zinazojitokeza ikiwemo vitisho tunazifahamu
, Na tunashukuru wanazisema wazi wazi , labda niwahakikishie wananchi
tumejipanga kuzikabili ili zisileta madhara kabla na baada ya uchaguzi
huo ”alifahamisha .
Kamishna
Hamdan pia ameeleza kwamba Jeshi limejipanga pia kubadilisha mfumo wa
kusimamia ili changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi uliofanyika 25,
oktoba mwaka jana wazigeuze kuwa fursa .
Akizungumza
ulinzi katika maeneo ya Visiwa Vidogo vidogo , amesema kwamba
watawatumia Askari shehia kutoa taarifa ili waweze kuyafikia maeneo yote
huku akisisitiza kwamba namba Za Simu za makanda wa Polisi Mikoa yote
ziko wazi na zinafahamika na wananchi waliowengi .
“Sisi Tupo wengi na maeneo yote tunayafahamu , kwa hili tutawatumia zaidi
askari wetu wa Shehia na kikubwa zaidi ni kwamba makamanda wote wa mikoa
Zanzibar namba zao za simu ziko wazi muda wote wananchi wanatakiwa
kuwapigia na kuwaeleza changamoto zinazowakabili ”alieleza.
Hata
hivyo alisema kwamba Jeshi la Polisi litafanya kazi kwa karibu na
Serikali za Shehia kwa kuwatumia masheha na kamati zao kuhakikisha
taarifa zote za uvunjifu wa amani zinaripotia na zinachukuliwa hatua kwa
mujibu wa sheria .
No comments:
Post a Comment