SDL RAUNDI YA 7
Raundi ya saba ya Ligi Daraja la
Pili nchini (SDL) inaendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa
nchini, kwa timu 24 kusaka pointi kutoka makundi ya A,B,C na D kuwania
nafasi nne za juu ili kuweza kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Kundi A, Leo Ijumaa Abajalo Tabora
watakua wenyeji wa Mvuvumwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Green
Warriors dhidi ya Singida United uwanja wa Mabatin Mlandizi (jumatatu)
na Mirambo FC watacheza dhidi ya Transit Camp siku ya jumatatu uwanja wa
Ali Hassani Mwinyi mkoani Tabora.
Kundi B, Kesho Jumamosi AFC ya
Arusha watakua wenyeji wa Alliance Schools uwanja wa Sheikh Amri Abeid,
Madini FC watacheza dhidi ya JKT Rwamkoma uwanja wa Mbulu, huku
Bulyanhulu FC watawakaribsiha Pamba FC uwanja wa Kamabrage mjini
Shinyanga.
Kundi C, Leo Ijumaa Abajalo Dar
watacheza dhidi ya Mshikamano uwanja wa Karume jijini Dar es salaam,
kesho Jumamosi Kariakoo FC watawakaribisha Changanyikeni katika uwanja
wa Ilulu – Lindi, na Cosmopolitani watacheza dhidi ya Villa Squad siku
ya jumatatu katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Kundi D, Jumamosi Mighty Elephant
watacheza dhidi ya Wenda FC uwanja wa Majimaji Mjini Songea, Mbeya
Warriors watawakaribisha Mkamba Rangers uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,
huku Jumapili Sabasaba FC wakicheza dhidi ya African Wanderers uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
STARTIMES LEAGUE RAUNDI YA 1
Na Kalonga Kasati
Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) Raundi ya 13 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 24 [kucheza michezo 12 katika viwanja tofauti, huku kundi A na C kukiwa na ushindani mkali kwa kila timu kuwania kupanda ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.
Kundi A, African Lyon
watawakaribisha Polisi Dar katika uwanja wa Mabatini – Mlandizi, Ashanti
United dhidi ya KMC uwanja wa Karume, huku Jumapili Kiluvya
wakiwakaribisha Polisi Dodoma uwanja wa Mabatini – Mlandizi na Friends
Rangers wakicheza na Mji Mkuu uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Kesho Jumamosi, Kundi B Polisi
Morogoro watacheza dhidi ya Njombe Mji uwanja wa Jamhuri, Morogoro,
Kurugenzi FC dhidi ya JKT Mlale uwanja wa Wambi – Iringa, Burkinafaso
dhidi ya Lipuli na Kimondo watawakaribisha Ruvu Shooting kwenye uwanja
wa Vwawa – Mbozi.
Kundi C, Polisi Mara FC
watawakaribisha Panone FC uwanja wa Karume mjini Musoma, Geita Gold
watacheza dhidi ya JKT Oljoro uwanja wa Nyankumbu mjini Geita, JKT
Kanembwa watakua wenyeji wa JKT Oljoro uwanja wa Lake Tanganyika mjini
Kigoma, huku Rhino Rangers wakicheza dhidi ya Mbao FC uwanja wa Ali
Hassani Mwinyi mjini Tabora.
LIGI KUU YA VODACOM RAUNDI YA 18 WIKIENDI HII
Na |Kalonga Kasati
Ligi Kuu ya Vodacoma Tanzania bara raundi ya 18 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, Jumamosi ukichezwa mchezo mmoja na Jumapili kuchezwa kwa michezo saba.
Jumamosi
ligi ya kuu ya Vodacom itaendelea kwa mchezo mmoja tu, ambapo katika
uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, African Sports watawakaribisha Stand
United kutoka mkoani Shinyanga.
Michezo
saba itachezwa siku ya Jumapili ambapo maafande wa JKT Ruvu watakuwa
wenyeji wa Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, na
Ndanda FC watawakaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Nangwanda
Sijaona mjini Mtwara.
Kagera
Sugar watacheza dhidi ya Simba SC katika uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga, Azam FC watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa Chamazi, Majimaji
dhidi ya Mgambo uwanja wa Majimaji mjini Songea na Toto Africans
watawakaribisha Coastal Union uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula kwenye jengo la Utalwala la Bunge
mjini Dodoma Februari 5, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Longido, Onesmo Ole-
Nangole kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Simanjiro , James Ole
Millya (kulia)kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016.
Katikati ni Mbunge wa longido, Onesmo Ole Nangole.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (katikati) na
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Patrobas katambi
(kulia) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwenye
viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016.
No comments:
Post a Comment