
Nyama ya nguruwe ni kitoweo ambacho kinapendwa na watu wengi nchini huku mahitaji yake ni zaidi ya tani 2000 ambapo asililimia kubwa huagizwa kutoka nchi za nje hii ni kutokana na uzalishaji mdogo wa ndani
Tafiti zilizofanyika hivi karibuni zinaonyesha kuwa nyama nyeupe ambazo hupatrikana na kuku na nguruwe zitakuwa na soko kubwa baada ya kufuatia udogo wa maeneo ya malisho na migogoro kwa mifugo aina ya ngombe mbuzi na kondoo ambao hutoa nyama nyekundu.
Kutokana na changamoto ya ubora wa mbegu za nguruwe wanaopatikana nchini chama cha wafugaji wa nguruwe Tanzania TAPIFA kimeamua kuagiza mbegu za kisasa kutoka nchi za Zambia, afrika ya kusini na ambayo imeonekana kuwa bora zaidi kwa kuzalisha nguruwe wenye kilo zaidi ya 100 katika kipindi cha miezi sita.
No comments:
Post a Comment