Sunday, 11 December 2016

EATV AWARDS itafanya Rais aendelee kuniacha- Nape

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo za EATV AWARDS zilizofanyika usiku wa tarehe 10 Desemba 2016 Mlimani City alifunguka na kusema kazi waliofanya EATV
na tuzo za EATV AWARDS anaamini kuwa hata Rais Magufuli ataendelea kumuacha acha kidogo katika wizara hiyo.
Waziri Nape alisema hayo wakati akimkabidhi Dj Bonny Love tuzo ya heshima na kusema kazi kubwa iliyofanywa na waandaaji wa tuzo hizo itamfanya mpka Rais Magufuli aendelee kumuacha acha kidogo kwani anaonekana na yeye akifanya kazi vyema.
"Kwanza napenda kuwapongeza waandaaji wa tuzo hizi kiukweli mmefanya kazi nzuri sana, kwa kazi nzuri hii lazima Mhe. Rais Magufuli ataendelea kuniacha acha kidogo kwani anaona nikifanya kazi" alisema Waziri Nape Nnauye
Mbali na hilo Waziri Nape Nnauye aliwataka watanzania kuwa wavumilivu na kusema wataacha kubana kama ambavyo amekuwa akiaambia mtaani kuwa wamebana sana hivyo milango itafunguliwa na mambo kuwa sawa mtaani.
"Tutaachia kidogo hatutabana sana, na mimi nimepita mtaani nimeambiwa Nape mmebana sana. Wakati wmingine tunataka kufanya mambo tunaambiwa tumepitiliza ila wakati mwingine tutafunga jicho moja watu wapitilize ili mambo yaende sawa sawa". Waziri Nape Nnauye

No comments:

Post a Comment