Alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape
Nnauye amewaomba radhi viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini
kwa lolote ambalo aliwakwaza wakati akitekeleza majukumu yake katika
nafasi hiyo.
Nape Nnauye (Kushoto) akiwa Edward Lowassa wakiteta jambo
Nape amewaangukia wapinzani pamoja na makundi mengine ya watanzania
ikiwemo viongozi wenzake ndani ya chama leo wakati akikabidhi rasmi
ofisi kwa kiongozi mpya anayechukua nafasi hiyo, ambaye ni Mkuu wa
Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam, Humphrey Polepole katika ofisi ndogo za
makao makuu ya chama hicho, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
"Nawaomba msamaha viongozi wenzangu, wanachama, waandishi na hata
wapinzani pale ambapo nimewaumiza katika kufanya kazi yangu, samahani
sana. Nategemea ushirikiano niliopatiwa mimi na wanahabari utaendelea
kwa ndugu yangu Humphrey Polepole, ni mtu mwenye weledi mpana" amesema
Nape
Nape pia amekiri kuwa chama hicho kimemsaidia zaidi kwenye maisha yake
kuliko yeye alivyokisaidia wakati akiitumikia nafasi hiyo.
"Nakiri mbele yenu kuwa chama kimenisaidia zaidi kuliko mimi
nilivyokisaidia Chama, nashukuru Mungu kuwa nimemaliza kazi hii salama,
nilipata wosia wa Mzee Kinana kuwa nishukuru nikimaliza salama"
No comments:
Post a Comment