Monday, 18 April 2016

Thomas Ulimwengu Anazidi Kuzifuma Nyavu


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu anaendelea kung’ara katika klabu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kongo, baada ya usiku wa Alhamisi kufunga bao katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Shark XI FC.

 

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliochezwa kwenye Uwanja wa Martys mjini Kinshasa, Ulimwengu alifunga bao hilo dakika ya 68 baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Rogger Asale dakika 57.

Ulimwengu alifunga bao hilo akimalizia pasi ya Rainfrod Kalaba, wakati bao la kwanza la Mabingwa hao wa Afrika lilifungwa na Luyindama dakika ya 65 kwa pasi ya Joseph Bolingi. Mazembe inarejea Lubumbashi kujiandaa na mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco Aprili 20 mwaka huu.

Mazembe inahitaji ushindi wa 3-0 ili kusonga mbele baada ya kufungwa mabao 2-0 katika Mchezo wa kwanza mwishoni mwa wiki mjini Casablanca.

No comments:

Post a Comment