Wednesday 27 April 2016

Said Miraji:ADC Kuna Watu Wenye Uchu wa Madaraka Wanaotaka kuharibu Taswira Njema ya Chama kwa Maslahi Yao Binafsi

 Na Chrispino Mpinge

Kuna usemi usemao “hakuna rafiki wa kudumu kwenye siasa na hakuna adui wa kudumu Kwenye siasa, na wengine wanasema siasa ni mchezo mchafu”. Semi hizi zina maana kubwa Sana Na hii inatokana na mabadiliko ya wanasiasa kwa kufuata upepo.

Hivi karibuni Chama Cha Allience For Democratic Change (ADC) kiliingia kwenye mgogoro Baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Said Miraj kuifuta Idara ya Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama iliyokuwa inasimamiwa na Omari A. Costastine, ambapo mwenyekiti huyo alifanya Hivyo kwa Mujibu wa Tamko la vyama vya siasa kutoviruhusu vyama kuwa na vikundi vya Ulinzi na Usalama.

Maamuzi Hayo ya Mwenyekiti Said Miraj Yaliipelekea Bodi ya Wadhamini kutoutambua Uongozi wa Said Miraj na kuunda Kamati Tendaji, jambo lililopelekea Mwenyekiti kupeleka Malalamiko hayo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, ambapo ametoa maamuzi ya kumtambua Mwenyekiti wa chama hicho na kueleza kuwa kwa Mujibu wa Katiba ya ADC Bodi ya Wadhamini haina Mamlaka ya kuufuta Uongozi wa chama hivyo Maamuzi hayo ni batili.

Hivyo Mwenyekiti huyo wa Chama cha ADC Said Miraji amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kusimamia maamuzi yake ambayo yanakiukwa na Bodi ya wadhamini, huku Akieleza kuwa bodi hiyo inaitisha vikao vya chama kinyume na katiba ya ADC inayohitaji Ridhaa ya Kamati Kuu ya Uongozi.

Vilevile ameongeza kuwa ADC imevamiwa na watu wenye Uchu wa Madaraka Wanaotaka kuharibu Taswira Njema ya chama, kwa Maslahi yao Binafsi bila kufuata Taratibu na Sheria Za Chama hicho.

No comments:

Post a Comment