Friday 29 April 2016

Uwekezaji Kati ya Tanzania na Urusi

Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akifungua kongamano la kujadili Fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jana jijini Dar es salaam ambalo limewakutanisha wafanyabiashara mbalimbali wa Mataifa hayo mawili. 
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage Akifafanua kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu faida za ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Urusi Utakaochangia maendeleo katika sekta za Kilimo, Usafirishaji na Nishati hapa nchini.
Waziri wa Viwanda na Biashara wa Urusi Mhe. Denis Manturov Akizungumza kwenye kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jana Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na urusi wakifuatilia mada wakati wa kongamano hilo  Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Bw. Reginald Mengi jana  Jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (wanne kutoka kushoto) akiwa na Wawakilishi wa Serikali ya Urusi, anayefuata ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage akifuatiwa na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum

No comments:

Post a Comment