Thursday 28 April 2016

Maafisa wa Serikali Watahudhuria Katika Mazishi ya Papa Wemba

Mamia ya watu wamejitokeza kuupokea mwili wa marehemu papa Wemba

Mamia ya watu Wamefurika  nje ya Uwanja wa Ndege wa Kinshasa kuupokea Mwili wa Mwanamuziki Papa Wemba Uliowasili nchini humo kutoka Abidjan

Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa Mmoja ya Waanzilishi wa Muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya Mwili huo kuwekwa katika Uwanja wa Mpira kwa Raia kutoa Heshima zao za Mwisho.

Maafisa wa Serikali na Wadiplomasia Watahudhuria ibada ya kumkumbuka Mwanamuziki Huyo katika Uwanja wa ndege kabla ya Mwili huo kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti.

No comments:

Post a Comment