Monday 25 April 2016

Historia ya Uchaguzi wa Mwaka Jana Hautafutika Vichwani Mwa Watanzania Walio Wengi

 

 Na Kalonga Kasati

Katika historia ya Siasa za Tanzania mwaka 2015 Umeweka Historia katika Uchaguzi Mkuu Uliofanyika Oktoka Ukihusisha Wabunge, Madiwani na Rais.

Mchuano Ulikuwa Mkali Baada ya Vyama vya Upinzani kuungana na kumsimamisha Mgombea Mmoja wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, Chini ya Mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) huku mgombea wa Chama Tawala (CCM) Dk. John Pombe Magufuli, akipata Upinzani Mkali Baada ya Wapinzani kuunganisha Nguvu na Kuwa kitu kimoja.

Nchini Marekani Mtia nia wa Chama cha Republican, Donald Trump amekumbana na Upinzani wa Baada ya Viongozi Wanaowania Nafasi Moja kutangaza kuungana ili kukabiliana Na Mgombea huyo.

Seneta wa Jimbo la Texas, Ted Cruz na Gavana wa Ohio, John Kasich Wametangaza Rasmi kuungana ili kumuwekea vikwazo Trump ambaye anakubalika katika Majimbo Mengi hadi Sasa, huku akikabiliwa na changamoto ya kupata Wajumbe Wanaohitajika kumpa Ushindi kabla ya Kongamano Kuu la Kitaifa la Chama Julai mwaka huu.

No comments:

Post a Comment