Friday 22 April 2016

Pluijim:Naamini Timu Yangu ina Nafasi Kubwa ya Kuingia Hatua ya Makundi

 

 Na Chrispino Mpinge

kOCHA wa timu yanga pluijm amesema anaamini timu yake ina nafasi kubwa ya kutinga Hatua ya makundi, hivyo atafanya kila linalowezekana kuhakikisha dhamira yake inatimia, Huku akitamba ana kikosi imara, isipokuwa kilikosa bahati mbele ya Al Ahly ya Misri, Katikati ya wiki hii.

Usiku wa Jumatano iliyopita, Yanga ilitolewa kwa jumla ya mabao 3-2 na Al Ahly kwenye Mchezo wa raundi ya pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1, kwenye mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Borg El Arab, jijini Alexandria, Misri.

 Pluijm alisema matumaini hayo yanatokana na ari na ubora iliyokuwa nao kikosi chake Ambacho kilipambana kufa kupona katika mchezo na Al Ahly, licha ya kutolewa kwenye Michuano hiyo.

“Siwezi kuwadharau wapinzani wetu Esperanca, lakini naamini hawatakuwa bora kama ilivyokuwa kwa Al Ahly na kama hivyo ndivyo basi, kuna uwezekano mkubwa kwa Yanga Kucheza hatua ya makundi kwa sababu tupo kwenye kiwango bora hivi sasa,” alisema kocha Huyo raia wa Uholanzi, lakini mwenye uzoefu mkubwa na soka ya Afrika.

Esperanca inayomilikiwa na Shirika la Taifa la Madini la Angola, inanyota kadhaa akiwemo `Babu’ mwenye umri wa miaka 37, lakini mwenye makali ya upachikaji mabao, Arsenio Sebastiao Cabungula maarufu kama Love ambaye mwaka 2006 alikuwa miongoni mwa nyota Wa Angola waliocheza Kombe la Dunia nchini Ujerumani.

No comments:

Post a Comment