Friday 29 April 2016

Donald Trump Kuwa Gumzo Mitandao Baada ya Kukosea Kutamka Tanzania Vizuri


Donald Trump kuwa gumzo mitandaoni baada ya kukosea kutamka Tanzania vizuri
Mgombea Urais wa Chama cha Republican Donald Trump amekejeliwa Mtandaoni Baada ya kuonekana akiboronga akitamka Tanzania Wakati wa kutoa Hotuba.

Bw Trump alikuwa akizungumzia Mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa katika Mabalozi ya Marekani nchini Kenya na Tanzania Mwaka 1998 Wakati wa kuzungumzia Sera yake ya kigeni.

Badala ya kutamka vyema ‘Tanzania’ anasikika akitamka ‘Tan-zay-nia’.

Mashambulio Hayo yalitekelezwa na Mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda.
Msemaji wa ikulu ya White House pia alimcheka Bw Trump alipoulizwa kuhusu vile Mfanyabiashara huyo Tajiri kutoka New York alivyotamka Jina Tanzania.

“Kweli, yamkini Jinsi ya kutamka huwa haijaelezwa kwenye kifaa cha kuonesha Maandishi ya Hotuba,” alieleza Afisa wa Habari wa ikulu Bw Josh Earnest.

No comments:

Post a Comment